KIFO CHA NGWEA: LADY JAYDEE NAYE ASITISHA SHOW YAKE
Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, mwanadada Judith
Wambura Maarufu kama Lady Jaydee ametangaza kuahirisha shughuli ya
maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika
Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge
kupisha msiba wa kifo cha msanii Albert Robert Mangweha aliyeripotiwa
kufariki nchini Afrika Kusini jana.
Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
Jaydee
ameeeleza uamuzi wake wa kutitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi
kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea
kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe
nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.
Tangu amekaribishwa
studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonzi sana kiasi cha
kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na
kukabwa na kilio.
No comments:
Post a Comment