TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, May 28, 2013

ARSENAL HATARINI KUMKOSA JOVETIC 
arsenal 2f412
 Mchezaji anayetakiwa kwa muda mrefu Arsenal, Stevan Jovetic wa Fiorentina anauzwa Pauni Milioni 25
 arsenal2 828b9
 Andrey Arshavin (kushoto), akiwa mazoezini na Jack Wilshere, anaweza kutimkia Zenit St Petersburg
MPANGO wa Arsenal kumsajili Stevan Jovetic uko hatarini kubuma kwa sababu zile zile mashuhuri za klabu hiyo ya London, 'ubakhili uliotukuka'.
Arsenal imeshindwa kutoa dau la Pauni Milioni 25 ambalo Fiorentina wanataka ili kumtoa Jovetic.
Mazungumzo baina ya klabu hizo mbili yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadhaa sasa, baada ya kocha Arsene Wenger kumfanya Jovetic mchezaji nambari moja katika orodha ya nyota anaowataka kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.
Lakini mpango huo unaelekea kugonga mwamba kutokana na klabu hiyo ya Serie A kugoma kuchukua kiasi chochote cha fedha chini ya Pauni Milioni 25 walizotaka.
Mabosi wa Gunners, wameiambia Fiorentina wako tayari kulipa tu Pauni Milioni 20 ili kumsajili mshambuliaji huyo wa Montenegro na kuna wasiwasi Juventus nao wanamnyatia Jovetic.
Kama Arsenal, vigogo hao Italia nao wameanzisha mazungumzo na klabu yake juu ya kumsajili Jovetic — lakini inafahamika itakuwa jambo gumu kwa Fiorentina kuwauzia silaha
wapinzani wake.

Pamoja na hayo, Juventus wako tayari kutoa dau ambalo Fiorentina wanataka, ili kuwabadilisha mawazo yao.

Wakati huo huo, Andrey Arshavin, ambaye amemaliza mkataba wake, anatakiwa na Zenit St Petersburg.
Mshika Bunduki huyo 'aliyetepeta', ambaye analipwa Pauni 90,000 kwa wiki, pia ana za kwenda kucheza Marekani na Mashariki ya Kati. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment