RAIS REAL MADRID AMPELEKA RONALDO CHELSEA
Ronaldo
Ronaldo akiwa na Mourinho
RAIS wa zamani wa Real Madrid, Ramon
Calderon amekuza matumaini ya Cristiano Ronaldo kufuatana na Jose
Mourinho Chelsea... baada ya kupuuza nafasi ya Manchester United
kumsajili tena nyota huyo Mreno.
Ronaldo, mwenye umri wa miaka 27, yuko
kwenye kinyang'anyiro cha kununuliwa kwa Pauni Milioni 80, baada ya
kuchoshwa na maisha katika Jiji la Hispania.
Alipoulizwa kama 'kipepeo' huyo wa
Ureno alikuwa ana furaha Real Madrid, Calderon alisema: "Ronaldo amesema
alikuwa ana machungu mwanzoni mwa msimu. Nafikiri uhusiano wake na rais
wa sasa si mzuri, labda kwa sababu rais hapendi wachezaji aliowakuta.
"Si timu nyingi zinazoweza kumlipa
kile anachostahili na pia itakayoweza kuilipa Real Madrid kile
wanachotaka. Kuna klabu tatu - Manchester City, PSG na Chelsea. Sifikiri
klabu yoyote nyingine inaweza kulipa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya
mchezaji".
"Wao (Real) wanakwenda kujadili
mkataba sasa na watafanya uamuzi. Ni kitu ambacho kitajulikabna ndani ya
wiki chache,"alisema.United ina nafasi ya kwanza ya kumsajili Ronaldo
ikiwa Real itaamua kumuuza nyota huyo wa Ureno itampa kipaumbele cha
kurejea Old Trafford. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment