TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, May 25, 2013

ASERNAL MBIONI KUSAJILI BEKI WA KATI
KLABU ya Arsenal imeripotiwa kukubaliana na vipengele vya uhamisho wa usajili wa beki wa kati wa Swansea, Ashley Williams katika zoezi ambalo litafungua milango ya kuondoka kwa Thomas Vermaelen Emirates.
 Kocha Arsene Wenger anavutiwa mno na Williams, ambaye anaweza kujiunga na Gunners msimu ujao.
Arsenal ilijaribu bila mafanikio kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Wales Januari mwaka huu na na inataraji kufufua mpango wake huo wiki zijazo, lakini Ijumaa ya leo Mwenyekiti wa Swansea, Huw Jenkins amekanusha kufanya mawasiliano yoyote na klabu hiyo.
Beki Mbelgiji, Vermaelen anahofia ndoto zake za kucheza Kombe la Dunia zinaweza kuyeyuka kama atabaki Arsenal msimu ujao.
Nahodha huyo wa Arsenal amesugua benchi miezi miwili ya mwisho huku Laurent Koscielny na Per Mertesacker wakicheza kama mabeki pacha wa kati.

No comments:

Post a Comment