MALUMBANO YA CUF NA CHADEMA BUNGENI YASABABISHA KIKAO KIAHIRISHWE KABLA YA WAKATI
Nukuu kutoka JF:
JF:Kufuatia
hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha cCUF kuwa ni chama cha
kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita CHADEMA ni wehu, wahuni,
wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha CUF.
Mbunge
huyo wa CUF ameomba Spika achukue hatua za dhidi ya CHADEMA asipofanya
hivyo CUF watachukua hatua dhidi ya CHADEMA na Bunge.
Kumetokea vurugu bungeni ambapo Spika ameliahirisha Bunge hadi jioni.
Quote:
By Tumaini Makene
Kipengele
kinachowasumbua katika hotuba ya Wenje ni hiki hapa...ambacho kimejaa
facts na ukweli. Wakanushe hizi facts. Wajibu hoja si kumshambulia mtoa
hoja. That is what argumentation is all about, let alone critical
thinking....
Kitu gani si cha kweli hapa?
3.0. VYAMA VYA SIASA NA MISAADA KUTOKA NJE YA NCHI.
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa 'United
Nations University'(UNU-WIDER) ya mwezi Aprili 2012 iliyoandaliwa na
Aili Mari Tripp ilionyesha kuwa misaada ya wahisani kutoka nje katika
mabadiliko ya kisiasa Tanzania 'Donor Assistance and Political Reform in
Tanzania', inaonyesha kuwa Tanzania imepokea misaada kutoka nje yenye
thamani ya dola za kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka 1990-2010.
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza
kusini mwa jangwa la Sahara kwa kupokea misaada mingi kutoka nje ya nchi
na hasa kutoka mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za Uingereza,
Marekani, Ujerumani, Uholanzi, Norway, Canada, Sweden, na taasisi kama
Benki ya Dunia, IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo.
Pamoja na
misaada yote hiyo, bado tumeendelea kuwa nchi maskini sana duniani
pamoja na kuwa na rasilimali lukuki ambazo tumepewa na Mungu ila
tunashindwa kuzitumia kwa manufaa ya watanzania na badala yake
tumeendelea kudanganywa na vimisaada vidogo vidogo na kubadilishana na
rasilimali zetu kama madini, misitu ,wanyama nk kwa ajili ya misaada
hiyo.
Mheshimiwa
Spika, pamoja na misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM bado vyama vya
siasa vimekuwa na mahusiano na baadhi ya vyama vingine vya siasa katika
mataifa ya magharibi na vimekuwa vikipokea misaada ya aina mbalimbali
kama fedha , nyenzo na mengineyo kadiri ya makubaliano na mirengo ya
kiitikadi ya vyama husika.Pamoja na ukweli huo bado vipo vyama vya siasa
vinavyopotosha umma kuhusiana na misaada vinayopokea kutoka nje ya nchi
na vyama hivi vimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda za uongo kuwa
vyenyewe havipokei misaada kutoka nchi za magharibi.
Mheshimiwa
Spika, CCM wao 'wanajiita' kuwa wapo mrengo wa kijamaa/kikomunisti na
wamekuwa wakipokea misaada mingi sana ya fedha na nyenzo kutoka Umoja wa
Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni 'Socialist International' kutoka
katika nchi kama za Ujerumani kupitia SDP ,Uingereza kupitia chama cha
Labour,China kupitia chama cha Kikomunist ,Marekani kupitia chama cha
Democrats. Pamoja na misaada ya kifedha na kiufundi ambayo CCM imekuwa
ikipata kutoka nje wamekuwa hawatangazi hadharani hata mara moja
kuhusiana na kiasi ambacho wamekuwa wakipokea na hivyo kila kitu kwao
imekuwa ni siri kuu ya viongozi wao.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo
wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na
"kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga". Hii ni kwa
mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali
ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza,
Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama
hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la
kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja,
wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre
cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha
Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana
na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine
mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa
mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama
cha Kiliberali kutoka Norway.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya
Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni
umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake
mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii,
ikimaanisha kwamba: "tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji".
Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika
serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party
cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata
mrengo huo.
Mheshimiwa
Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo
vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na
malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa
vikipokea kutoka kwenye nchi hizo .
No comments:
Post a Comment