CHELSEA YATWAA EUROPA LEAGUE YAINYUKA BENFICA 2-1
Chelsea
Torres akishangilia bao
Patrick Kluvert akiingia na kombe uwanjani
Torres akichezewa rafu
Baada ya kuvuliwa ubingwa wa ligi ya
mabingwa barani ulaya walioutwaa mwaka jana, kukosa ubingwa wa England
na kombe la FA nchini Uingereza, hatimaye wazee wa London, klabu ya
Chelsea wamefanikiwa kupunguza machungu baada ya kutwaa ubingwa wa ligi
ya Uropa usiku wa kuamkia leo.
Chelsea wameifunga Benfica 2-1 katika
mchezo wa fainali na shukuruni za pekee ni kwa beki wake Branislav
Ivanovic aliyefunga bao dakika ya lala kwa buriani (Dakika 93) na
kumpatia kocha wake wa muda Rafa Benitez atakayeondoka baada ya msimu
huu na kumpisha kocha mwingine anayesemekana kuwa Jose Mourinho.
Hakika ubao wa matangazo wa dimba la
Amsterdam mpaka dakika ya 90 ulikuwa unasomeka 1-1 na watu wengi
wakaamini timu hizo zinaenda kutumia sheria nyingine ya mashindano.
Wakati watu wakijiandaa kupata dakika
nyingine, Ivanovic alichafua hali ya hewa kwa Benfica na kuleta furaha
kubwa sana kwa mashabiki wa Chelsea waliosafiri kutoka London mpaka
Uholanzi kuwashangilia vijana wao.
Haikuwa kazi nyepesi kwa Chelsea
kushinda mchezo wa jana usiku, lakini jinsi walivyoonekana kujituma muda
wote walionesha kuwa na umoja mkubwa sana huku Kocha Benitez
akiwahamasisha muda wake ili kubeba ndoo na kuondoka kwa amani. Channzo:
sportmail
No comments:
Post a Comment