UFAFANUZI KUHUSU LIGI YA MABINGWA MIKOANI
Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa (RCL) ilianza tarehe 12 Mei 2013 ikishirikisha klabu
bingwa za mikoa yote ya Tanzania Bara, isipokuwa mikoa ya Pwani na
Manyara ambayo kutokana na sababu tofauti ilishindwa kuwasilisha majina
ya klabu zake hadi siku ya mwisho iliyowekwa na Kamati ya Mashindano,
yaani tarehe 10 Mei 2013.
Suala la
kukosekana kwa wawakilishi wa mikoa hiyo miwili limezua maswali mengi
kiasi kwamba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linalazimika
kutoa ufafanuzi kwa faida ya wadau wote wa mpira wa miguu.
Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa, ambayo ni mpya baada ya TFF kubadilisha mfumo wa
uendeshaji wa mpira wa miguu, ilipangwa kuanza tarehe 5 Mei 2013, lakini
hadi tarehe ya mwisho ya kuwasilisha majina ya mabingwa wa mikoa, yaani
tarehe 2 Mei 2013 mikoa michache ndiyo iliyokuwa imemaliza ligi zao na
kupata mabingwa.
Kuchelewa
huko kwa mikoa kumaliza ligi zao kuliilazimisha Kamati ya Mashindano ya
TFF kuongeza muda wa mikoa kuwasilisha majina ya wawakilishi hao hadi
tarehe 10 Mei 2013 na hivyo siku ya kuanza kwa Ligi kusogezwa mbele hadi
tarehe 12 Mei 2013.
Hadi
kufikia tarehe hiyo mpya ya mwisho ya kuwasilisha majina ya mabingwa wa
mikoa, ni mikoa sita tu iliyofaidika na kuongezwa huko kwa muda na
kupata wawakilishi wake. Mikoa hiyo ni Iringa, ambayo pamoja na
kuongezwa kwa muda, iliandika barua ya kuihakikishia Kamati ya
Mashindano kuwa itapata bingwa kabla ya kuisha kwa siku ya tarehe 10 Mei
2013.
Mikoa mingine ni Lindi, Mtwara, Geita, Tabora na Dodoma.
Mkoa wa Manyara haukuweza kumaliza ligi yake hadi mwisho wa siku ya tarehe 10 Mei 2013 na hivyo Kamati ya Mashindano iliyosubiri majina hadi saa 12:00 jioni siku hiyo kuamua kuwaondoa wawakilishi wa Manyara kwenye ratiba.
Mkoa wa Manyara haukuweza kumaliza ligi yake hadi mwisho wa siku ya tarehe 10 Mei 2013 na hivyo Kamati ya Mashindano iliyosubiri majina hadi saa 12:00 jioni siku hiyo kuamua kuwaondoa wawakilishi wa Manyara kwenye ratiba.
Awali,
Kamati ya Mashindano iliamua kuwa ratiba ya mechi za Ligi ya Mabingwa wa
Mikoa ipangwe tarehe 7 Mei 2013, ikishirikisha mikoa ambayo ilishapata
mabingwa wake, lakini baada ya kuona baadhi ya mikoa ilikuwa
haijakamilisha ligi zake, Kamati iliamua kuwa ratiba ipangwe kwa kutumia
majina ya mikoa kwa matumaini kuwa hadi kufikia tarehe 10 Mei 2013,
mikoa itakuwa imeshapata wawakilishi wake na kwa kuwa ratiba inahusu
mikoa jirani, ingekuwa rahisi kwa timu kusafiri kutoka kituo kimoja hadi
kingine.
Lakini
Mkoa wa Manyara haukuweza kufanya hivyo na Kamati kulazimika kuuondoa
kwenye ratiba kutokana na kushindwa kukidhi utashi huo.
Mkoa
mwingine ambao uliondolewa kwenye ratiba ni Pwani ambayo pamoja na
kutuma jina la mwakilishi wake, Kamati ilipokea malalamiko kutoka klabu
zilizoshiriki Ligi ya Mkoa, zikidai kuwa jina la bingwa wa Pwani
lililowasilishwa TFF lilikuwa batili kwa kuwa klabu ya Kiluvia United
haikustahili kushiriki Ligi ya Mkoa kutokana na ukweli kuwa
haijasajiliwa mkoani Pwani na wala haikushiriki ligi ya mkoa msimu
uliopita. Kamati ya Mashindano iliiondoa Pwani kwenye ratiba na
kulirudisha suala hilo mkoani.
Ingawa
Katibu wa Pwani alijaribu kuishawishi Sekretarieti ya TFF iliangalie
suala hilo kwa undani zaidi, Sekretarieti ilimjibu kuwa lilishafanyiwa
uamuzi na Kamati, hivyo uamuzi huo usingeweza kutenguliwa na kumshauri
katibu huyo arejee mkoani kwake kuwasiliana na viongozi wenzake kuona ni
jinsi gani mkoa unaweza kunusuru hali hiyo kwa kufanya uamuzi ambao
ungeuwezesha mkoa kupata mwakilishi.
Kwa
mantiki hiyo, masuala ya Manyara na Pwani yalikuwa ndani ya uongozi wa
mikoa husika na si Kamati ya Mashindano ya TFF kwa kuwa Kamati ilitaka
ipatiwe jina la bingwa ambaye alipatikana kwa mujibu wa mfumo mpya wa
Ligi ya Mikoa.
Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na hivyo
timu zilizokutana tarehe 12 Mei 2013, zitarudiana mwishoni mwa wiki hii
na kupatikana timu zitakazosonga mbele kwenye raundi nyingine hadi timu
tatu bora zitakazopanda daraja kwenda Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
zitakapopatikana.
Ligi za
Mikoa, kwa mujibu wa kanuni mpya, zinatakiwa ziwe na timu kati ya 16 na
20 na zinatakiwa zicheze mechi mbili za nyumbani na ugenini, hata kama
zitakuwa zinatumia uwanja mmoja.
Uamuzi wa
kubadilisha mfumo huo ulifanywa ili kuhakikisha kuwa mikoa inakuwa na
na mashindano kwa mwaka mzima na hivyo kuiwezesha mikoa kujikita katika
kutafuta mbinu za kupata fedha na kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu
kwenye mikoa yao.
Uamuzi
huo pia unasaidia kupunguza mtindo wa wachezaji kuzunguka klabu tofauti
katika msimu mmoja kwa kuwa wanalazimika kutulia kwenye klabu moja hadi
muda wa usajili unapofika.
Pamoja na
wachezaji kutulia sehemu moja kwa muda mrefu, pia walimu wanapata fursa
ya kujikita vizuri kwenye programu zao kwa kuwa wanakuwa na uwezo wa
kufuatilia maendeleo ya wachezaji wao.
Pamoja na
hayo yote, mfumo huo utasaidia kurudisha msisimko kwenye mikoa na hivyo
kutoa fursa kwa vijana wengi wenye vipaji kuonekana na kuendelezwa.
TFF
inatoa wito kwa viongozi wa mikoa kuanza kubuni sasa mikakati ya
kuendesha ligi hizo msimu unaokuja kwa kuwa hakutakuwa na nafasi tena ya
kuongeza muda kwa mikoa kuwasilisha majina ya wawakilishi wao.
KIINGILIO MECHI YA SIMBA, YANGA 5,000/-
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 18 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 18 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa
upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi
ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B
itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja
itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi
wa mechi hiyo atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro ambapo atasaidiwa na
Samuel Mpenzu wa Arusha, na Jesse Erasmo kutoka Morogoro. Mwamuzi wa
akiba ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Leslie Liunda.
KOCHA KIM KUZUNGUMZIA MECHI YA MOROCCO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tiketi kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco. Mkutano huo utafanyika keshokutwa (Mei 16 mwaka huu) saa 5 kamili kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tiketi kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco. Mkutano huo utafanyika keshokutwa (Mei 16 mwaka huu) saa 5 kamili kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mechi
hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8 mwaka huu kwenye jiji la Marrakech
nchini Morocco. Taifa Stars ilishinda mechi yake iliyopita jijini Dar es
Salaa kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Morocco.
Angetile Osiah
Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment