WASANII WAAIRISHA SHOW ZAO KWA AJILI YA MSIBA WA ALBERT NGWEA
Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini akiwemo Mwana Fa, Izzo Business, pamoja na Kara Pina wamehairisha shoo zao ambazo zilikuwa zinatarajia kufanyika Mei 31 mwaka huu kwa sababu ya kifo cha msanii mwenzao Albert Mangwea kilichotokea jana nchini Afrika ya Kusini.
Mwana Fa ambaye alitarajia kufanya onyesho lake alilolipa jina la The Finest mwishoni mwa wiki hii amejikuta akiahirisha shoo hiyo kwa sababu ya msiba wa msanii mwenzao
Kwa upande wake Izzo Business alieleza sababu ya kuahirisha shoo hiyo, alisema kuwa hawezi kuendelea na ratiba ya shoo hiyo wakati yupo katika wakati wa majonzi kwa kumpoteza msanii wao ambaye pia ni rafiki yao mpendwa
No comments:
Post a Comment