WANYWAJI WAPINGA VIROBA KUPIGWA MARUFUKU
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji
walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited
(TDL), Dar es Salaam hivi karibuni.
Vikipigwa marufuku viroba tutarudi kunywa gongo
BAADHI ya
wananchi jijini Dar es Salaam, wamelalamikia hoja iliyozuka bungeni
wiki hii kwamba kinywaji cha Konyagi aina ya Kiroba kipigwe marufuku
nchini.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao, walisema endapo serikali itachukua
uamuzi wa kupiga marufuku kinywaji hicho, watarudia kunywa pombe aina ya
gongo ambayo ni hatari kwa afya zao.
Mkazi wa
Mbagala, Faustine Mwiruka aliyekutwa kwenye baa ya Kisuma, aliiasa
Serikali kutothubutu kukubali kinywaji hicho kupigwa marufuku, kwani
ikifanya hivyo wengi wa wananchi wenye kipato cha chini wataanza tena
kunywa gongo na pombe za kienyeji.
Itabidi
tufanye kama Zambia ambao wamezuia viroba, lakini nchi nzima imejaa
viroba vya Malawi, Zaire na Burundi, lazima tuiadhibu serikali ikose
kodi kote kote, bia hatunywi, viroba vya nje tutakunywa, pamoja na
gongo.
Alisema
haingii akilini kukihusisha kinywaji hicho na ajali za magari, akidai
kuwa hata kabla ya viroba kuingia sokoni ajali zilikuwepo nyingi.
"Sisi
tuna imani na viroba kwa vile vina ubora wa uhakika tofauti na pombe ya
gongo ambayo inapikwa bila kupimwa ubora hivyo ni hatari kwa usalama wa
afya zetu." alisema Mwiruka.
Naye Ali
Hassan mkazi wa Kinondoni kwa Manyanya, alisema, wanaotaka viroba
vipigwe marufuku hawawatendei haki wananchi wa kawaida ambao kwa
asilimia kubwa hawana uwezo wa kununua bia ambazo bei yake ni kubwa.
Mwandishi
wetu aliyetembelea maeneo ya Ilala Kota Mchikichini
alifanikiwakuhojiana na wakazi wa eneo hilo ambao wengi wao walisema
kuwa jambo hilo lililozushwa wiki iliyopita wanaamini ni njama za
wafanya biashara toka nchi jirani ambao hawaitakii mema Tanzania kwa
kuwa pombe hiyo kuwepo kwake pia kunakuza pato la Taifa.
Juma
Pingu alisema kuwa haoni sababu ya kupiga marufuku viroba kwakuwa ni
pombe ya wanyonge na kuwataka wabunge kuthamini bidhaa za nyumbani
kwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, Mkurungenzi Mkuu wa
Konyagi, David Mgwassa alisema kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwa na
mchezo mchafu wa kuharibiana jina sokoni kwa kutumia baadhi ya vyombo
vya habari vya hapa nchini, kampeni inayoendeshwa na makampuni yenye
uhusiano na makampuni makubwa ya pombe duniani yasiyo penda, nchi za
afrika zizalishe pombe zake, bali ziendeleee kununua kutoka Ireland,
wales. Kenya and uingereza.
Wadau hao
wa Pombe nchini walifikia uamuzi wa kutoa maoni hayo baada ya kuona
kuwa kinywaji chao Kiroba kinapigwa vita lukuki kwenye magazeti. Huwezi
ukahusisha viroba na piki piki, kwani nchi hii ina piki piki laki tatu,
na wananchi million 43, uhusiano wake uko wapi, kwanza hata leseni
hamuwapi?
No comments:
Post a Comment