TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, May 25, 2013

DAVID MOYES KULETA MSAIDIZI KUTOKA EVERTON,PHELAN NA STEELE WAJAA WASIWASI
man2 b7d3d
David Moyes na Sir Elex Ferguson

man3 3be76
Kocha wa makipa Eric Steele (wambele) anasemekana kutimka zake baada ya ujio wa David Moyes

man e1fdc
Mike Phelan aliteuliwa na Ferguson kuwa msaidizi wake septemba mwaka 2008

Kocha msaidizi wa mabingwa wa soka nchini Uingereza, Manchester United, Mike Phelan na kocha wa makipa, Eric Steele wamejawa na wasiwasi wakibarua chao kuota nyasi kufuatia ujio mpya wa kocha wa united David Moyes ambaye anasemekana ana mipango ya kumleta kocha mwenza wa Everton Jimmy Lumsden kuwa msaidizi wake katika safari yake ya kuifundisha klabu yake mpya.
Nafasi ya Phelan amekuwa hatarini tangu United imtangaze Moyes kuwa mrithi wa mikoba ya kibabu Alexndar Chapman Ferguson kwani kocha huyo anaonekana kuwa na nia ya kumleta kocha Lumsden ili kuenda sambamba kuijenga United mpya.
Moyes alikutana na Phelon jumanne ya wiki hii wakiwa na Ferguson, Steele na kocha wa sasa wa United Rene Muelensteen katika uwanja wa mazoezi wa Carrington ambapo Moyes alisema leo Ijumaa ataanika mipango yake pamoja na kumtaja msaidizi wake. Chanzo: Baraka Mpenja

No comments:

Post a Comment