KIEMBA ASAINI SIMBA,KASEJA MAZUNGUMZO YANAENDELEA
KIUNGO matata wa wekundu wa Msimbazi
Simba, Amri Athman Kiemba amekubali kuongeza mkataba wa kuichezea klabu
hiyo kwa msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Keptein Zacharia Hans Poppe amesema kuwa wameshazungumza na kukubaliana na Amri Kiemba jambo ambalo limewapa raha sana kutokana na ubora wa mchezaji huyo aliyekuwa akitajwa kuihama Simba na kujiunga na Yanga msimu ujao.
“Kuhusu Kiemba tumeshaziba midomo ya watu, amekubali kwa moyo mkunjufu kuitumikia klabu yake msimu ujao, ni bonge la mchezaji, tunafurahi kuwa nae katika kikosi chetu”. Alisema Poppe.
Kuhusu nahodha Juma Kaseja, Poppe alisema wanaendelea kuzungumza naye ili kumsainisha mkataba mwingine huku wakikubaliana kuboresha maslahi yake klabuni hapo.
Kuhusu suala la Shomary Kapombe, Poppe amewatoa mashabiki wa kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba na Simba hadi aprili mwakani na ataendelea kubaki msimbazi.
Wakati huo huo, Hans Poppe alisema zoezi la kuwasainisha mikataba mipya wachezaji wote wa timu hiyo linaendelea vizuri, ikiwemo wale waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, yaani Simba B.
Poppe aliongeza kuwa mwaka huu wanahitaji kufanya mambo yao kimya kimya ili kuwazuia wale wasiojua kusaka wachezaji ila wakijua Simba wamempa nani wanakimbilia kuwasainisha. Chanzo: Baraka Mpenja
No comments:
Post a Comment