YANGA YAZAWADIWA SH.25 M NA TBL KWA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU
Meneja wa kampuni ya bia ya TBL George
Kavishe akikabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 25 kwa katibu mkuu wa
Yanga Lawrence Mwalusako
Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania
bara na mabingwa watetezi wa kombe la Kagame, klabu ya Yanga ya Dar es
salaam wamepewa zawadi ya sh. Milioni 25 kutoka kwa wadhamini wakuu wa
klabu hiyo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wameizawadia klabu hiyo Sh.
Milioni 25 kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara uliomalizika mei 18
mwaka huu.
TBL, wanaoidhamini Yanga na Simba
kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi mfano wa hundi ya
Sh. Milion 25 leo kwa Yanga katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Safari
Pub, uliopo makao makuu ya TBL, Ilala, Dar es Salaam.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium
Lager, George Kavishe wakati akikabidhi mfano wa hundi hiyo alisema
Kilimanjaro Premium Lager imefurahishwa sana na ubingwa wa Yanga na
kusema imejizatiti kikamilifu kuisaidia timu ambayo imeibuka bingwa
katika ligi yenye ushindani mkubwa kutokana na kuibuka kwa timu mpya
zenye nguvu.
“Yanga imekuwa akionesha soka safi kwa
kipindi chote, ligi ni ngumu sana lakini wamecheza soka maridadi, hivyo
kuibuka mabingwa sio ajabau kabisa. Napenda kuwapongeza wachezaji wa
Yanga, kocha na Uongozi mzima wa Yanga kwa matokeo mazuri ya kushinda
Ligi kuu kwa mara ya 24 sasa.” Alisema Kavishe.
Kavishe aliongeza kuwa zawadi hiyo ni
sehemu ya sh bilioni 1.5 ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa
Yanga na imetolewa kwa lengo la kuhamasisha klabu kujitahidi kwa
ushindi zaidi na kusaidia klabu katika maandalizi yake kwa ajili ya
mashindano ya kimataifa ambayo tayari Yanga ina sifa za kushiriki
kutokana na ubingwa waliojipatia.
Akipokea hundi hiyo, Katibu mkuu wa
Yanga , Bwana Lawrence Mwalusako alisema Yanga inaishukuru sana
Kilimanjaro Premium Lager kwa mchango wao. Aliongeza kuwa Yanga ni timu
nzuri na yenye nguvu kutokana na uongozi imara pamoja na udhamini mkubwa
kwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
‘‘Mafanikio yetu ya uwanjani ni
kielelezo cha mafanikio ya kampuni na pia (TBL) na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager kwa ujumla ambayo imekuwa ikitusaidia sana.’’ alisema
Mwalusako.
Mwalusako aliongeza kuwa kwa sasa
Yanga ina nafasi ya kuonekana kwenye jukwaa la kimataifa la soka
kutokana na mafanikio hayo na kuahidi kujipanga zaidi kufanbya makubwa
zaidi.
Yanga itawakilisha Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Kagame. Chanzo: Baraka Mpenja
No comments:
Post a Comment