BAYERN BINGWA ULAYA YAICHAPA DORTMUND 2-1
Bayern
Mabingwa wa Ulaya, Bayern
Wajerumani si mchezo katika soka,
fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya imepigwa katika dimba la
Wembley jijini London usiku wa kuamkia leo ambapo kwa mara ya kwanza
timu mbili kutoka Ujerumani zimekutana katika mechi kali na ya kusisimua
baina ya wekundu wa kusini mwa ujerumani Bayern Munich na nyuki wa
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo Borrusia Dortmund.
Kwa kawaida mechi nyingi za fainali
huwa zinapigwa mpaka dakika 120 mpaka mikwaju ya penati kama ilivyokuwa
kwa mwaka jana ambapo Chelsea waliifunga Bayern, lakini fainali ya leo
imepigwa ndani ya dakika tisini.
Winga wa FC Bayern Mholanzi Arjen
Robben ameipatia klabu yake zawadi kubwa sana ya kutwaa ubingwa msimu
huu baada ya kufunga bao la pili na la ushindi katika dakika ya 88 ya
kipindi cha lala salama.
Bao hilo limetokana na kazi nzuri ya
winga mwenye kasi zaidi Frank Ribery aliyempa pasi nzuri Robben na
kupachika bao kiufundi zaidi.
Ubingwa huo ni wa tano kwa Bayern
ambao katika misimu minne wamecheza mechi tatu za fainali bila
mafanikio. Chanzo: Baraka Mpenja
No comments:
Post a Comment