MHE. PETER MSIGWA AACHIWA KWA DHAMANA
Msigwa akiwa amebwa juu juu na wanachama wa chadema mara baada ya kuachiwa kwa dhamana
Mamia ya wanachama wa chadema wakiandamana kuonyesha furaha yao ya kuachiwa kwa dhamana mhe: mbunge Peter Msigwa
Msigwa akiongea na wapiga kura wake mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.
Na Said Ng'amilo Iringa
MBUNGE wa Iring mjini Mch. Peter
Msigwa (CHADEMA) na wafanyabiashara 75 mapema leo walipandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Wilaya wakikabiliwa na makosa matatu .
Msigwa anakabiliwa na makosa mawili
ambapo kosa la kwanza ni la kwake pekee yake na huku kosa la pili
likiwahusu washtakiwa wote.
Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo
mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Godfrey Isaya, mwendesha mashta
wa serikali Adolf Maganda alisema Peter Msigwa ambaye ni mshtakiwa
namba moja anakabiliwa na shtaka la kushawishi watu kutenda uhalifu
ambapo alisema Msigwa alifanya ushawishi huo katika mkutano alioufanya
Mei 15 Mwaka huu katika maeneo ya mashinetatu.
Kosa la pili ambalo linawakabili
watuhumiwa wote 76 limetajwa kuwa watuhumiwa walifanya mkusanyiko pasipo
kibali cha polisi na kusababisha uhalibifu, ambapo alisema Mei 19 Mwaka
huu watuhumiwa walikusanyika katika maeneo ya mashine tatu bila kibali.
Akisoma kosa la tatu Maganda alisema
linawahusu watuhumiwa namba 2 hadi namba 76, alisema mnamo Mei 19 Mwaka
huu watuhumiwa waliharibu kwa makusudi gari lenye namba za usajili SM
9323 mali ya kikosi uokoaji na zimamoto Iringa.
Baada ya kusomewa makosa yao, wakili
wa kujitegemea Bazil Mkwata alisema makosa wanayokabiliwa nayo wateja
wake yanadhamana na hivyo kuiomba mahakama wateja wake wapewe dhamana.
Akitoa masherti ya dhamana hiyo,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Godfrey Isaya aliwataka washtakiwa kila
mmoja kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika ambaye anatakiwa kuwa na
shilingi milioni moja na kwamba washtakiwa hao wakipewa dhamana
wasijihusishe na uhalifu tena.
Hata hivyo mwendesha mashtaka huyo
alisema upelelezi haujakamilika na watuhumiwa 49 wapo nje kwa dhamana
baada ya kukidhi masharti ya dhamana, huku washtakiwa 27 wakirudishwa
rumande baada ya kukosa dhamana na kesi hiyo itatajwa tena Juni 3 Mwaka
huu.
Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani
siku moja baada ya kukamatwa katika purukushani za askari kuzuia
wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) kufanya biashara zao katika maneo
ya mashinetatu.
Aidha Katika mkutano wa kiserikali
uliofanyika 19 Mei Mwaka huu katika maeneo ya Mashinetatu Msigwa
alisisitiza Machinga kutoondoka katika maeneo hayo ili waweze kufanya
biashara kwa ajili ya kupata chochote kwa ajili ya familia zao.
Mara baada ya kutoka mahakamani
wafanyabiashara na wananchi walimbeba mbunge wao hadi ofisi ya chama
iliyopo Mshindo ambako aliongea na wnanchi.Akiongea na umati wa wananchi Msigwa aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano walio uonesha kwake na kwa wafanyabiashara tangu mwanzo wa tukio hadi mwisho, kwa kile alichosema wameonesha uzalendo wa dhati.
"Ninawashukuru sana wananchi kwa uzalendo wenu japo kuwa kuna watu wangu wamekosa dhamana lakini nawaahidi kuwa kesho (leo) nitafanya jitihada zote kwa kushirikiana na viongozi wenzangu kuwatoa. Ila niwatoe wasiwasi kuwa waliobaki watatoka" alisema Msigwa.
Kwa upande wao wafanyabiashara wamemfananisha Msigwa na Mwalimu Nyerere kwa moyo wake wa dhati na upendo wa kweli kwa kile walichosema kuwa anachokisema ndicho anachofanya.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment