STEVEN GERRARD KUFANYIWA UPASUAJI WIKI HII
Gerrard
Gerrard
Na Baraka Mpenja Kwa msaada wa Sportsmail.com
Msimu wa ligi kwa nahodha machachari
wa majogoo wa jiji, klabu ya Liverpool, Steven Gerrard umefikia
ukingoni baada ya kuthibitishwa kuwa nyota huyo anafanyiwa upasuaji
sehemu ya bega wiki hii.
Gerrard alitakiwa kufanyiwa upasuaji baada ya msimu kumalizika lakini klabu yake imesema imeamua kumfanyia zoezi hilo baada ya majeraha yake kuendelea kuwa makubwa.
Zoezi hilo la upasuaji litamfanya nyota huyo kukosa michezo miwili ya ligi kuu Engalanda na mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya Brazil mwezi ujao, pia atakosa mchezo dhidi ya Jamhuri ya Ireland mei 29 mwaka huu uwanjani Wembley.
Gerrard itahitaji miezi sita hadi nane kupona na Liverpool inatarajia kumtumia katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu.
Ratiba ambayo Gerrard atakosa
May 12 – Fulham v LiverpoolMay 19 – Liverpool v QPR
May 21 – Ajax Cape Town v Liverpool
May 29 – England v Republic of Ireland
June 2 – Brazil v England
No comments:
Post a Comment