BOMU LA ARUSHA: PENGO AFICHUA SIRI
Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.
"Jana
(juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na
imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa
nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia
ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa
kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,"
alisema Kadinali Pengo na kuongeza:
"Lengo la
msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa
nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano
na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu," alisema Pengo.
Alisema
kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi
ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila
kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.
"Tusipojua
kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu.
Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu
wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu
na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema
ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani," alisema Pengo.
Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.
"Naomba
kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa
letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika
atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo," alisema. :chanzo
Mwananchi
No comments:
Post a Comment