MCHEZO WA AC MILAN ,ROMA WASIMAMA KUTOKANA NA UBAGUZI WA RANGI
li

Mchezo ulisimama kwa muda sababu ya ubaguzi

Balotelli

Balotelli na Kevin Prince-Boateng wakiwa wamesimama pamoja wakati wa tangazo linatolewa uwanjani

Sulley Muntari alitolewa nje kwa kumsihi refa
Refa Gianluca Rocchi alisimamisha
mechi na mtangazaji wa uwanjani akawaambia mashabiki wa Roma waache
kuwafanyia ishara za nyani wachezaji weusi wa Milan, vinginevyo mechi
itaahirishwa.
Mapema Sulley Muntari alitolewa nje
kwa kadi nyekundu wakati anakwenda kumsihi refa huyo aliyeonekana aataka
kumpa kadi ya pili ya njano Balotelli.
Massimo Ambrosini alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokwenda kulalamika kwa refa Rocchi kabla ya mechi kusimamishwa.
Totti baadaye alitolewa nje kwa kadi
nyekundu kwa kumchezea rafu beki wa Milan, Phillipe Mexes na mechi hiyo
ikaisha kwa sare ya bila kufungana.
Mchezo wa kirafiki Januari baina ya
Milan na Pro Patria ulisimamishwa pia kwa sababu kejeli za kibaguzi
alizofanyiwa Kevin-Prince Boateng.
Shirikisho la soka Italia limeweka
sheria mpya kuwasaidia marefa kudhibiti ubaguzi baada ya kiungo wa
Milan, Kevin-Prince Boateng kuamua kuondoka uwanjani January katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Pro Patria baada ya kukutana na dhalili
hiyo. Chanzo:binzubeiry
No comments:
Post a Comment