BARCA YASHEREKEA TAJI KWA KUIFUNGA ALTETICO MADRID 2-1

Wachezaji wa Barcelona wakishangilia taji la La Liga

Nyota wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas na Alex Song wakishangilia kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Barcelona

Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya Lionel Messi kutoka

Radamel Falcao akishangilia bao lake
PAMOJA na kwamba Lionel Messi
alishindwa kucheza jana kutokana na kusumbuliwa na maumivu, lakini
haikuzuia Barcelona kushinda 2-1 dhidi ya Atletico Madrid usiku wa jana
na kushangilia taji la 22 la Ligi Kuu Hispania.
Messi alianza katika mechi ya kwanza
ndani ya raundi sita kwa sababu ya kusumbuliwa na maumivu ya nyama za
paja la kulia, lakini akaondoka uwanjani dakika ya 68 Barcelona ikiwa
nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Radamel Falcao dakika ya 52 na Barca
ikakamilisha wachezaji wote watatu wa kubadilisha.
Hata hivyo, Alexis Sanchez
akasawazisha dakika ya 72 na kiungo wa Atletico, Gabi Fernandez
akajifunga dakika ya 80 hivyo kuamsha pati la ubingwa kwa Barcelona,
wakiivua rasmi ubingwa Real Madrid.
Mapema siku hiyo, Valencia ilijiongezea matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Rayo Vallecano.
Roberto Soldado alifunga mabao mawili
kabla ya mapumziko, wakati Andres Guardado na Nelson Valdez
wakakamilisha karamu ya mabao kipindi cha pili.
Huo ulikuwa ushindi wa pili mfululizo
wa 4-0 kwa Valencia na unamaanisha timu ya Ernesto Valverde inaizidi
kwa pointi moja Real Sociedad, ambayo leo itakuwa mwenyeji wa Granada.
Malaga na Sevilla zote zina nafasi ya
kucheza michuano ya Ulaya baada ya sare ya bila kufungana uwanja wa La
Rosaleda. Chanzo:Binzubeiry
No comments:
Post a Comment