TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, May 10, 2013

HALMASHAURI ZATAKIWA KUBUNI VYANZO VYA MAPATO
SERIKALI inatambua  kazi kubwa zinazofanywa na wenyeviti  wa vijiji na vitongoji katika kuhimiza na kusimamia  shughuli  za maendeleo  kwenye maeneo yao.
Serkali inapeleka rasilimali fedha ,vifaa na rasilimali watu kwa wingi  katika mamlaka ya Serikali  za Mitaa.Uamuzi huu wa Serikali  umesaidia kuwapa fursa  wananchi kujiwekea  vipaumbele   vya utekelezaji  wa miradi  ya maendeleo  kwa kuzingatia  fursa na vikwazo  vilivyopo.
“Viongozi  hawa wana majukumu ya kuhamasisha ushiriki  wa wananchi  katika uchangiaji wa miradi  ya Maendeleo  na kusimamia  utekelezaji  wa miradi hiyo kupitia kamati za maendeleo  za vijiji “ alisema  Naibu Waziri wa Fedha  Janet Mbene kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Aidha Naibu huyo  aliendelea kwa kusema kwamba ,kwa kutambua uzito wa majukumu  haya ,Serikali kupitia  kila Halmashauri  imeweka utaratibu  wa kuwalipa posho  wenyeviti wa vijiji  na Mitaa kutokana na vyanzo vya mapato ya ndani ambayo ni asilimia 20 ambapo kati ya hizo asilimia 3 ni fedha  za maendeleo  na asilimia 17  ni kwa ajili ya ya shughuli  za utawala  ikiwemo kulipa posho.
Hata hivyo ,viwango  ambavyo hulipwa  vinatofautiana  kati ya halmashauri moja na nyingine  kulingana na uwezo  wa kukusanya mapato ya ndani katika vyanzo vilivyopo.
Aidha changamoto  kubwa inayoikabili ni ufinyu wa bajeti  pamoja na makusanyo kidogo  katika halmashauri
.Aidha ,mkazo umekua ukitolewa  kwa halmashauri  zote nchini  kuhakikisha kuwa asilimia 20  ya mapato ya ndani ya  halmashauri  zinapelekwa  katika vijiji ,kuimarisha  ukusanyaji wa mapato ya ndani  na kubuni vyanzo  vipya vya mapato. Chanzo: Immaculate Makikila, Dodoma

No comments:

Post a Comment