Wajumbe wa Baraza la usalama wataka uwajibikaji kwa mzozo Sudan Kusini
Baadhi
ya watoto huko Sudan Kusini mustakhbali wao uko mashakani kutokana na
mapigano yanayoendelea nchini mwao. (Picha: UNMISS/Tina Turyagyenda.
Wajumbe
wa baraza la usalama waliopatiwa fursa ya kuchangia hoja baada ya
kuwasilishwa kwa ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu Sudan Kusini
wamesema kinachoendelea hakikubaliki na ni aibu kubwa.
Mapigano
ya wenyewe kwa wenyewe Sudan Kusini yalianza tarehe 15 Disemba mwaka
jana kati ya vikosi vya serikali na vile vinavyomuunga mkono Makamu Rais
wa zamani Riek Machar.
Mmoja
wa wajumbe hao ni Mwakilishi wa kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa
Mataifa Balozi Eugene Richard Gasana ambaye amesema matumaini yaliibuka
wakati wa uhuru wa Sudan Kusini mwaka 2011..
(Sauti ya Balozi Gasana.)
"Hata
hivyo miaka mitatu baadaye na kwa kuzingatia kuenea kwa mauaji ya raia
pamoja na hali ya haki za binadamu kama ilivyoelezwa na watoa ripoti wa
leo na pia kusisitizwa na Balozi Samantha, hatuwezi kubakia watazamaji
tu. Huwezi kugombania uhuru kwa miaka na baadaye kugeuka na kuanza kuua
raia wako wewe mwenyewe. Ni aibu!"
Mwakilishi
wa Kudumu wa Uingereza Balozi Mark Lyall Grant akasema ripoti za Bi.
Navi Pillay na Adama Dieng zimeweka dhahiri ukiukwaji wa haki za
binadamu na akaunga mkono hatua za Muungano wa Afrika na IGAD za kupatia
suluhisho la mapigano yanayoendelea. Balozi akatoa mapendekezo. (CHANZO:UM REDIO) (FS)
No comments:
Post a Comment