USIOMBEE KUUGUA DENGUE KIPIMO SH.50,000
Wakati
taharuki iliyosababishwa na mlipuko wa homa ya dengue ikiendelea
kutikisa kila kona ya jiji, imebainika kwamba gharama za vipimo katika
hospitali mbalimbali zinafikia Sh50,000, ikiwa ni tofauti kubwa na
Sh1,000 kwa kipimo cha malaria.
Ugonjwa
huo unazidi kusambaa jijini Dar es salaam na baadhi ya mikoa, kiasi cha
mamlaka kuagiza mabasi yote yaendayo mikoani yafanyiwe usafi wa
kunyunyizia dawa za kuua wadudu kudhibiti usienee zaidi mikoani. Pia
wananchi wameshauriwa kuvaa nguo ndefu ili kudhibiti mbu wanaoeneza
ugonjwa huo mchana tofauti na mbu wa malaria.
Timu ya
waandishi wa Mwananchi ilipita katika baadhi ya hospitali kubwa binafsi
na za Serikali jijini Dar es Salaam na kubaini kuwa gharama ya kupima
homa hiyo ni kubwa zaidi katika hospitali na vituo binafsi vya afya,
lakini wagonjwa wanaokwenda katika hospitali za Serikali hulazimika
kulipa kati ya Sh25,000 na Sh30,000. Pamoja na homa hiyo kufananishwa na
malaria kwa dalili na kuenezwa na mbu, gharama za vipimo vyake ni
tofauti kwani mgonjwa wa malaria hutozwa kati ya Sh1,000 na 2,000.
Hata
hivyo, jambo la kutia moyo ni kwamba baada ya mgonjwa kupata majibu na
kubainika anaumwa homa ya dengue, gharama za tiba huwa ndogo kati ya
Sh200 na 500 za kununulia dozi ya dawa za kutuliza maumivu aina ya
panadol.
Wanaopima waongezeka(P.T)
Mchunguzi
wa magonjwa katika maabara ya kimataifa ya Lancet, Kanda ya Tanzania,
Mohamed Abdulai alisema idadi kubwa ya watu wanakwenda katika maabara
hiyo kupima homa ya dengue tangu ugojwa huo uenee kwa kasi kati ya Machi
na Aprili mwaka huu.
Alisema
kwa siku wagonjwa zaidi ya 40 hupima dengue na katika kipindi
kisichozidi mwezi mmoja, wagonjwa 53 waligundulika kuwa na homa hiyo.
Abdulai alisema gharama za kipimo cha dengue katika kituo hicho ni Sh50,000.
Katika
Hospitali ya Aga Khan, Mkurugenzi wa Tiba, Dk Jaffer Dharsee alisema
kipimo cha homa ya dengue ni kati ya Sh35,000 hadi Sh40,000 kutokana na
mchakato wa upimaji wake.
"Ni
lazima tunapompima mtu dengue pia tumpime na maradhi mengine kwanza kama
homa ya matumbo, malaria na maradhi mengine ambayo tunahisi anayo na
ndiyo gharama inakuwa kubwa," alisema Dk Dharsee.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Hindu Mandal, Dk Kaushik Ramaiya alisema katika
hospitali hiyo kipimo cha homa ya dengue ni Sh30,000. "Tunatumia vipimo
vitatu, kile kitakachoangalia iwapo chembe hai nyeupe za damu
zimepungua, malaria na kiwango cha sumu kinachotokana na virusi vya
dengue," alisema.
Dk
Ramaiya alisema tangu vyombo vya habari vianze kuripoti ugonjwa huu,
watu wamejawa hofu na hufika hospitali kwa wingi wakitaka kupima maradhi
hayo ili kujua kama wapo salama
No comments:
Post a Comment