Sentensi 6 za Askofu wa kanisa lililolipuliwa bomu Mwanza
Miongoni mwa stori kubwa za AMPLIFAYA ya CloudsFM wiki hii ni hii ya bomu kulipuliwa kwenye kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Mwanza ambapo lilijeruhi mtu mmoja alielazwa hospitali ya Bugando.
- Mkuu wa dayosisi Askofu Andrew Gulle anasema ‘May 5 2014 bomu limelipuka katika usharika wa kanisa kuu Imani kwenye eneo la rest house saa mbili usiku, ni bomu la kutengenezwa kwa mkono na lilikua limewekwa kwenye karatasi za kufungia zawadi na kuwekwa kwenye mfuko wa plastiki na kuwekwa kwenye varanda ya rest house yetu’
-
‘Kifurushi hicho kimekuwepo kuanzia siku ya Ijumaa ambapo ilipofika
Jumatatu saa mbili usiku muhudumu wa rest house Benadertha alianza
kujiuliza kifurushi hicho kina nini na kwanini kimekuwepo hapo kwa siku
tatu? ambapo mwishowe aliamua kukifungua ili kujua kuna nini ndani
lakini ghafla bomu lililipuka kwa kishindo na moshi mwingi huku
likisambaza misumari midogomidogo na kumjeruhi miguuni na usoni’
3. ‘Alikimbizwa hospitali ya rufaa ya Bugando na kufanyiwa upasuaji na kulazwa kwenye wodi ya mifupa, hatujui lengo la wahusika lilikua kumuumiza yeye au wengi zaidi, au walishindwa kulifikisha walipotaka lifike?
- ‘Vikao vya kanisa vimekaa kutafakari na sasa natamka kama kiongozi wa Dayosisi yale tuliyokubaliana kuyasema kwa Watanzania…… tunalaani kitendo hicho kilichofanyika kwenye eneo la Kanisa, tunaomba makanisa yetu kuboresha ulinzi katika maeneo yetu yote kwa sababu hatuwezi kujua watu hawa wamekusudia kuweka mabomu wapi na wapi’
No comments:
Post a Comment