TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, May 21, 2014

Dengue kuwakumbusha usafi wa Mazingira


Mwanza. Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Kebwe Stephen amewataka viongozi wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanasimamia utunzaji mazingira ili kukabilina na ugonjwa wa Dengue ambao umeshika kasi Dar es Salaam. (J M)
Pia, Dk Kebwe amewagiza viongozi wa mkoa huo kukutana na viongozi wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Kanda ya Ziwa, kuanza mara moja kupulizia dawa kwenye mabasi yanayoingia na kutoka mkoani hapa.
Akifungua mpango wa uzazi kwa kutumia nyota ya kijani mkoani hapa jana, Dk Kabwe alisema kutokana ugonjwa wa Dengue kusambaa kwa kasi Dar es Salaam, Serikali imedhamiria kuhakikisha ugonjwa huo hauinei mikoa mingine. Alisema wameanza kutoa elimu na kuwagiza viongozi wa Serikali za mikoa kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo kwenye mikoa yao.
“Nimekuja Mwanza kwa lengo la kuhakikisha tunapambana na ugonjwa wa Dengue, Dar es Salaam tumeanza kwa kupulizia dawa kwenye magari ya abiria na mitaa mbalimbali, naomba vingozi wa hapa mkutane na Sumatra na kwamba mara moja utaratibu huo uanze,”alisema Dk Kebwe na kuongeza:
“Kesho (leo) mkutane na kuanza kuweka mkikakti hiyo, naomba agizo hili lizingatiwe kuhakikisha ugonjwa huu hausambai Kanda ya Ziwa,”alisema.
Dk Kebwe alisema ugonjwa huo unaenezwa na mbu aina ya Aedes mosquito, ambao hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus.
“Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo, naomba wananchi mjikinge kwa kuvaa nguo ndefu, kufukia mashiomo ya majitaka na utunzaji mazingira, Serikali imejipanga kuhakikisha ugonjwa huo hausambia maeneo mengine ya nchi,”alisema.
Dk Kebwe aliwataka wakazi wa Mkoa wa Mwanza kutumia njia za uzazi wa mpango, kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na kutozingatia uzazi wa mpango.
Dk Kebwe alisema wametenga Sh3 bilioni kwa ajili ya kuboresha masuala ya uzazi wa mpango, lengo likiwa ni kuhakikisha wanapunguza vifo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga alisema takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kati vizazi hai 100,000, wanaofariki kwa matatizo ya uzazi ni 454. CHANZO MWANANCHI

No comments:

Post a Comment