Kupima Virusi vya Ukimwi ni jambo la hiari
Na Ali Issa Maelezo -Zanzibar
Kupima
Virusi vya Ukimwi linabaki kuwa jambo la hiari kwa muhusika na
linaweza kuwa ni kitu cha lazima iwapo Daktari au Mahakama wamefikia
maamuzi ya kufanya hivyo kwa sababu maalum ya kupatiwa ufafanuzi wa
jambo. (FS)
Hayo
yamesemwa jana huko Baraza la Wawakilishi Mbweni, nje kidogo ya mji wa
Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais Fatma
Abdulhabib Fereji wakati akijibu suali la Mwakilishi Jaku Hashimu
Ayoub alieitaka Serikali kuwalazimisha wananchi kupima virusi vya
ukimwi kwa kuanzia viongozi wa Serikali na Wanasiasa.
Alisema
Zanzibar ni Sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo
imeridhia mikataba ya Kimatafa na Kikanda na kuheshimu haki za
Binadamu, hivyo Zanzibar inawajibu wa kuzingatia na kutekeleza kwa
vitendo maazimio ya Ulimwengu ambayo yanakataza kuwalazimisha watu
kupima ukimwi.
“Muongozo
wa Shirika la Kazi Duniani juu ya masuala ya ukimwi ni sehemu za kazi
na linapinga kuwalazimisha watu kupima virusi vya ukimwi hasa
wanapotaka kuomba kazi au shurutisho kwa waajiriwa,”alisema Waziri
Fatma.
Aidha
Waziri huyo alisema kua kushurutisha upimaji wa virusi vya ukimwi ni
njia mojawapo ya kuwanyanyapaa na kuwabagua watu waishio na hivyo na
hilo pia ni kinyume na sera za nchi na Mikataba ya Kimataafa dhidi ya
ugaguzi.
Hata
hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais alisema sera ya
Taifa ya 2006 imeweka miongozo tosha ya upimaji virusi vya ukimwi kwa
lazima pale ambapo Mahakama na Hospitali zitalazimika kufanya hivyo kwa
mujibu wa sheria.
“Hatua
hii itafanyika iwapo pametokea udhalilishaji wa kijinsia na ubakaji,
naomba nisisitize kwamba suala la ajira, nafasi za uongozi wa kisiasa na
Serikali halikuwekewa ulazima wa kuchunguza virusi vya ukimwi,”
aliongeza Waziri.
Pamoja
na hayo Waziri Fatma alisema Baraza la Wawakilishi lilipitisha mswada
wa sheria desemba 2013 wa kuweka masharti ya kukinga na kusimamia
masuala ya ukimwi Zanzibar kulinda na kuheshimu haki za watu wanaoishi
na virusi vya ukimwi..
No comments:
Post a Comment