SHERIA YA KIJESHI YATANGAZWA THAILAND
Jeshi la
Thailand limetangaza kuweka sheria za kijeshi katika juhudi za kurejesha
utulivu wakati nchi hiyo imekumbwa na mzozo wa kisiasa kwa muda.
Jeshi hilo pia limejitwika nguvu nyingi zaidi ili kuweza kutekeleza sheria hiyo.
Hata
hivyo Jeshi hilo, ambalo lilinyakua mamlaka mnamo mwaka wa 2006 limesema
kuwa hatua yake sio mapinduzi bali ni hatua ya kudhibiti usalama wa
taifa.
Sheria hiyo ya kijeshi imekuja kufuatia mvutano wa muda mrefu wa kisiasa kati ya serikali na upinzani.
Bado tuko uongozini
Mshauri mkuu wa masuala ya usalama kwa kaimu waziri mkuu, amesema kuwa hawakushauriwa juu ya hatua hiyo.
Bwana
Paradorn Pattanatabut amesisitiza kuwa kila kitu kinaendelea kama
kawaida isipokuwa tu jeshi limedhibiti masuala yote ya usalama nchini
humo.
Wanajeshi
wameshika doria katika sehemu muhimu za nchi ikiwemo eneo ambapo
wafuasi wa serikali wamekuwa wakiandamana nje kidogo ya mji mkuu
Bangkok.
Tunataka demokrasia
Wafuasi
hao wa serikali wamesema kuwa wataendelea na maandamano yao hadi utawala
wa kidemokrasia utakaporejeshwa. Misuko suko imemzonga waziri mkuu huyo
wa Thailand kwa muda huku akiamrishwa na mahakama ajiuzulu.
Upinzani
pia umekuwa ukisisitiza kuwa unataka uongozi wa nchi ukabidhiwe kwa bodi
ya usimamizi ambayo haikuchaguliwa kidemokrasia, ambayo kwa sasa
inasimamia masuala ya marekebisho ya katiba.(P.T)
No comments:
Post a Comment