MAREKANI KUSAIDIA NIGERIA KWA WASICHANA
Marekani
imetangaza kwamba imetuma kikosi cha wataalamu nchini Nigeria kusaidia
kuwatafuta wasichana takriban 200 wa shule waliotekwa nyara mwezi
uliopita na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Rais
Barack Obama ameshutumu utekaji nyara wa wasichana hao na kusema kuwa
mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kulikomesha Boko Haram.
"Tayari
tumetuma kundi letu Nigeria. Wamekubali msaada wetu ambao unashirikisha
wanajeshi, wadumishaji wa sheria na mashirika mengine ambao wanajaribu
kutambua waliko wasichana hawa ili wawape msaada," Rais Obama alisema.
Rais
Obama amesema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kutumia utekeji wa
kikatili wa wasichana hao kama msingi wa kuungana na kuangamiza Boko
Haram.
Nchini Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amekubali msaada huo kama alivyosema msemaji wake, Daktari Reuben Abati.
"msaada
huo kutoka kwa Rais Obama uliwasilishwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni
John Kerry kama saa tisa alasiri hivi," Daktari Abati alisema.(P.T)
No comments:
Post a Comment