TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, May 9, 2014

MAREKANI 'INAIFUNGIA MLANGO'SYRIA

131022102952_suriah_304x171_ap_nocredit_2681b.jpg
Marekani imeiwekea vikwazo benki moja ya Urusi inayofanya biashara na Syria kama sehemu ya jitihada za kuzidisha shinikizo za kiuchumi dhidi ya serikali ya Syria
Hatua hiyo ilitangazwa wakati viongozi wa upinzani walioitembelea Washington wameanza kukutana na maafisa wakuu wa utawala.
Hii ni mara ya kwanza Marekani imeiwekea vikwazo benki ya Urussi inayofanya biashara na Syria.
Maafisa wa hazina ya Marekani wanasema hatua hii inanuiwa kuifungia milango Syria isiweze kuendelea kupenya mfumo wa kifedha wa dunia.
Vikwazo zaidi pia vimewekewa viwanda kadhaa vya kusafisha mafuta pamoja na maafisa sita wa ngazi ya juu katia serikali ya Syria.
Hayo yalitangazwa mda mfupi tu kabla ya kiongozi wa upinzani wa serikali ya Syria Ahmad Jarba alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa wa Marekani John Kerry.
Ahmad Jarba yuko katika ziara ya kwanza rasmi huko Marekani ambako anatarajiwa pia kukutana na rais wa Marekani Barack Obama.CHANZO BBC(A.I)

No comments:

Post a Comment