BONDIA COSMAS CHEKA AHAIDI KUTETEA TAJI LAKE VIZURI
Cosmas Cheka 'kulia' 
 Na Mwandishi Wetu
 BONDIA 
Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni Juni Mosi kwa ajili ya kutetea 
taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja 
katika ukumbi wa vijana socil hall  wa Morogoro.
 
Akizungumzia mpambano huo Cheka amesema amejiandaa kupigana kawa raundi 
kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni bondia 
huoyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Fransic Cheka ambaye alikuwa
 bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe amesema yeye anataka afike mbali 
zaidi ya kaka yake huyo.
 Mpambano
 huo utakaosimamiwa na TPBO utasindikizwa na mapambano ya utangulizi 
kati ya Kudura Tamimu atakae vaana na Sadiki Yusufu wakati Mohamed 
Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu 
 Siku 
hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia 
wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic
 Miyeyusho,Japhert Kaseba Vs Thomas Mashali .Floyd Mayweathar,Manny 
Paquaio, Saul 'canelo' alverez, Mike Tyson, Mohamed Ali, Ferex Trinidad,
 Miguel Cotto na wengine wengi.
 DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D.'
 Pamoja 
na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na 
vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na
 Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za 
Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia 
watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi.
No comments:
Post a Comment