TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, May 7, 2014

Taarifa ya Jeshi la Polisi Dodoma kuhusu Vurugu zilizotokea Mei 05 Kibaigwa

nomaaa
Kutoka Dodoma Mei 05 majira ya saa saba mchana kulitokea vurugu zilizoanzishwa na wabeba mizigo wa Mji mdogo wa Kibaigwa ambapo taarifa inasema zilikua ni vurugu zilizosababisha magari kadhaa kuvunjwa vioo.
Miongoni mwa magari yaliovunjwa vioo ni pamoja na la Mbunge wa Tanga Omary Nundu,gari la Polisi na basi linalofanya safari zake kati ya Dar na Mwanza la Shabaha mbali na kuvunjwa kwa magari hayo pia maduka yaliporwa na hata barabara kuu ya Dodoma-Morogoro ilifungwa.
misimeee
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amesema David Misime amesema Mpaka sasa jeshi la polisi linawashikiliwa watu 34 ambao ni wakazi wa kibaigwa kata ya kibaigwa wilaya ya kongwa kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu mali.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo inasema vijana zaidi ya 300 wakishirikiana na wabeba mizigo wa Kibaigwa walifanya maandamano yasiyo na kibali na kung’oa bango la halmashauri ya kongwa lililokua na tangazo la kukataza wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru.
Baada ya bango hilo vijana hao waliamua kufunga barabara kuu ya Dodoma Morogoro kwa mawe na kuchoma matairi baadae walivamia maduka na kupora vinywaji na kuvunja majokofu.
Chanzo cha vurugu hizo  ni wabeba mizigo wa soko la mazao Kibaigwa  kupinga kitendo cha Halmashauri ya Kongwa kuweka tangazo la kutoza ushuru wa mazao sokoni hapo wakidai kwamba inawakosesha kufanya kazi zao kwani wateja wao wanashindwa kuingiza mazao sokoni.

No comments:

Post a Comment