TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, July 14, 2013

VAN PERSIE ATUA SYDNEY KUIONGEZEA NGUVU MAN UNITED
van 79caf
Mshambuliaji wa Man United, Robin van Persie (HM)
KOCHA David Moyes ameongezewa nguvu katika timu yake, baada ya mshambuliaji Robin van Persie kuungana na kikosi cha Manchester United mjini Sydney kwa ajili ya mchezo wa pili wa ziara ya kujiandaa na msimu.
Mholanzi huyo, ambaye aliwafungia mabao 30 Mashetani Wekundu katika msimu uliopita, alipewa muda maalum wa kuungana na tomu tofauti na wenzake, baada ya kumaliza kuitumikia timu yake ya taifa, Uholanzi na akakosa mechi ya kwanza ambayo United walifungwa 1-0 Singha All-Stars mjini Bangkok jana.
Timu ya Uholanzi ilikwenda katika ziara bara la Asia, mwezi Juni, ambako walizufunga timu za China na Indonesia, huku van Persie akicheza mechi zote.
Itakuwa nafasi yake ya kukutana kwa mara ya kwanza na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes, aliyerithi mikoba Sir Alex Ferguson aliyestaadu baada ya msimu uliopita. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment