TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, July 14, 2013

THIAGO ALCANTARA AJIUNGA NA BAYERN MUNICH,AKITOSA MAN UNITED
article-2362924-1AC45694000005DC-357 634x4581 80677
Thiago Alcantara amesaini mkataba wa miaka minne Bayern (HM)
art cbc37
HATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Spain na FC Barcelona Thiago Alcantara ameuzwa rasmi kwenda kujiunga na mabingwa wa ulaya na Ujerumani Bayern Munich.

Thiago ambaye alikuwa akihusishwa mno na kujiunga na Manchester United ingawa juzi kocha David Moyes alisema hawakuwahi kusema wanamhitaji mchezaji, amejiunga rasmi ya Bayern Munich kwa ada ya uhamisho wa 25 million euros.

Mapema wiki iliyopita kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola alikaririwa akisema kwamba anamhitaji Thiago kwenye timu yake na amewaomba viongozi wake kumsajili mchezaji huyo tu msimu huu. Thiago amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea Bayern Munich.
Alizaliwa Italia na wazazi Wabrazil, kabla ya kujiunga na akademi ya Barcelona alikofundwa soka ya kitaalamu hadi mwaka 2008 alipoanza kucheza. 

Kiwango cha Thiago kimefanya azitoe mate klabu kadhaa kubwa Ulaya, ikiwemo United, na Guardiola aliripotiwa akisema kiungo huyo ni mchezaji nambari moja anayemtaka majira haya ya joto.

Aling;ara na kuiwezesha Hispania kutwaa Kombe la Ulaya la U21, akifunga Hat-trick katika fainali dhidi ya Italia

Guardiola alimpandisha Thiago timu ya kwanza misimu miwili iliyopita na alicheza mechi 45, lakini maumivu yalimpunguzia idadi ya mechi hadi 36 msimu uliopita chini ya kocha Tito Vilanova, Barcelona ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Hispania. 

Pamoja na kuchezesha timu vizuri, kuwa na uwezo wa kupiga chenga na kufumua mashuti ya mbali, hakuweza kuwa chaguo la kwanza katika safu ya kiungo ya Barcelona mbele ya akina Andres Iniesta, Xavi Hernandez na Cesc Fabregas. Chanzo: sportmail

No comments:

Post a Comment