TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, July 10, 2013

MOYES AANZA MAZOEZI NA MAN UNITED WAKIWEMO ZAHA NA ROONEY
new 98a7f
Kocha wa Man United, David Moyes (HM)

2 a824e
KOCHA mpya wa mabingwa wa soka nchini England, Mashetani wekundu wenye makazi yao katika dimba la Old Trafford, David Moyes ameanza maisha yake mapya akiwa na United badala ya Everton na leo hii amewaweka pamoja wachezaji wake katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington akiwaongoza kufanya mazoezi.
Moyes aliambatana na msaidizi wake Steve Round tofauti na kocha aliyemrithi mikoba, Sir Alex Ferguson ambaye alikuwa anasaidiwa na  Mike Phelan pamoja na Rene Meulensteen na kuifanya United kuwa timu bora kwa muda mrefu.
Nyota asiyetabirika kwa sasa kama atabaki United au la!, Wayne Rooney, nyota mpya aliyesajiliwa Wilfried Zaha na kocha mchezaji, mkongwe Ryan Giggs ni miongoni mwa wachezaji waliohudhuria katika jalamba hilo la kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England.

No comments:

Post a Comment