MIKOA YATAKIWA KUWASILISHA RATIBA YA COPA COCA-COLA
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), linavitaka vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwasilisha ratiba
zao za michuano ya U15 Copa Coca-Cola kabla ya Julai 15 mwaka huu. (HM)
Ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa
16 pekee ambavyo npyo vimewasilisha TFF ratiba hizo mpaka sasa. Jumla ya
mikoa 32 ya Tanzania Bara na Zanzibar inashiriki katika michuano hiyo
ya umri chini ya miaka 15 kuanzia ngazi ya wilaya ambapo ngazi ya mikoa
inatakiwa kuanza Julai 15 mwaka huu.
Mikoa ambayo tayari imewasilisha
ratiba zao ni Arusha, Ilala, Kagera, Kaskazini Pemba, Kaskazini Unguja,
Kigoma, Kinondoni, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Manyara, Mara, Mjini
Magharibi, Morogoro, Singida, Tanga na Temeke.
Wakati huo huo, WASH UNITED YAKABIDHI FULANA 200 KWA KLINIKI YA TFF
Taasisi ya Wash United
inayojishughulisha na usaji na utunzaji mazingira imeikabidhi fulana 200
na dola 1,000 za Marekani kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano kati yake na TFF
yaliyosainiwa Novemba mwaka jana.
Fulana hizo kwa ajili ya kliniki za
kila wikiendi (Jumamosi na Jumapili) zinazoendeshwa na TFF katika vituo
20 nchini kikiwemo cha Karume ikiwa ni sehemu ya mpango wa grassroots
unaoshirikisha watoto wa umri kati ya 6 na 17 zimekabidhiwa na Mratibu
wa Wash United, Femin Mabachi.
Hafla ya kukabidhi msaada huo
imefanyika leo (Julai 9 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF ambapo kwa upande
wake ulipokelewa na Ofisa Maendeleo wake Salum Madadi.
Wash United inafadhiliwa na Serikali
ya Ujerumani kupitia shirika lake la maendeleo la GIZ, na hapa nchini
moja ya eneo wanalotumia katika kampeni hiyo ili kupambana na magonjwa
kama kuhara yanayosababishwa na uchafu ikiwemo kutonawa mikono vizuri,
hivyo kusababisha vifo kwa Watanzania ni mpira wa miguu. Chanzo:
Boniface Wambura
No comments:
Post a Comment