Ukiwa unakaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa mara ya kwanza kabisa
chaneli ya 4 ya televisheni ya nchini Uingereza itakuwa ikirusha hewani
moja kwa moja adhana ya sala ya asubuhi.
Justine Bower mkurugenzi
wa masuala ya umma wa chaneli ya 4 ya televisheni ya nchi hiyo amesema
kuwa, kanali hiyo itakuwa ikirusha moja kwa moja adhana ya asubuhi kwa
ajili ya wananchi wa Uingereza.
Ameongeza kuwa, waumini wa dini ya
Kiislamu wapatao milioni mbili na laki nane nchini humo wataanza mfunguo
wa mwezi mtukufu wa Ramadhani siku chache zijazo. Bower amesema kuwa
kanali hiyo pia itakuwa ikirusha hewani adhana kupitia mtandao wa kanali
hiyo.
Alipoulizwa wamejiandaa vipi kukabiliana na ukosoaji kwa
hatua hiyo, Justine Bower amesema kuwa, karibu asilimia 5 ya wananchi wa
nchi hiyo wako katika pilika pilika za kuukaribisha mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Amesema kuwa, mwezi wa Ramadhani hufungwa na waumini wa dini
ya Kiislamu kila mwaka, na nitawashangaa watu watakaostaajabishwa na
uwepo wa utambulisho huo wa kidini.
No comments:
Post a Comment