CHRISTINA SHUSHO AIWEKA TANZANIA KWENYE HEADLINE AFRICA NZIMA
Mkali wa gospel Tanzania Christina Shusho
ambaye anafanya vizuri na wimbo wa Napenda, amekuwa na mwaka mzuri sana
kwa upande wa kazi zake za kimuziki. Kama ulikuwa hujui mkali huyu
anakubalika sana kwenye nchi za jirani ya Tanzania hasa Kenya. Miezi
kadhaa iliyopita kwenye moja ya event ya utoaji wa awards kubwa za
gospel nchini Kenya maarufu kama Groove Awards ambazo pia zilihidhuriwa
na Rais wa kenya Uhuru Kenyatta na mke wake, Christina Shusho alishinda
award ya msanii bora wa gospel wa Tanzania akiwashinda wakali wenzake
kama Rose Muhando na wengine.
Kubwa zaidi ni iliyo happen wiki hii, Christina Shusho ameshinda
award kubwa za gospel ambazo zinahusisha wasanii wote wa africa, Kwenye
category ya Best Gospel artist from East Africa ambapo kulikuwa na
wasanii lukuki ndani yake. List inahusisha wasanii kama FABRICE
NZEYIMANA.ALICE KAMANDE.EXODUS-UGANDA,CHRISTINA SHUSHO TANZANIA,BLESSED
SISTERS RWANDA,GEN. MANASSEH MATHIANG SOUTHERN SUDAN,JOY NKUNDIMANA
BURUNDI,JULIANI,EMMY KOSGEI,MOSES “QQU” ODHIAMBO,DADDY OWEN
na MARVELLOUS. Watu wangu gospel mtakuwa mashajua jinsi gani list hii
ina watu wakali sana. Lakini Christina Shusho anastahili pongezi za
pekee kwa kushinda tuzo hii na kuiwakilisha Tanzania vema kwenye anga ya
muziki wa injili.
No comments:
Post a Comment