WIGAN BINGWA KOMBE LA FA YAICHAPA MAN CITY 1-0

Kombe la FA likiwasilishwa uwanjani

Joe Hart akiruka bila mafanikio

Makocha wa Man city na Wigan wakati wote wa mchezo walikuwa na hekaheka

Ben Watson akishangilia bao lake la ubingwa wa FA
BAO la Ben Watson katika dakika ya
mwisho kabisa jioni hii limeipa Wigan ubingwa wa Kombe la FA kwa mara ya
kwanza kabisa ikiichapa Manchester City 1-0 kwenye Uwanja wa Wembley.
Nyota huyo aliyetokea benchi alifunga
kwa kichwa akiunganisha kona na kuwa shujaa wa mashabiki wa Wigan na
kumfanya Roberto Mancini arejee nyumbani mikono mitupu.
Man City ilimaliza pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Zabaleta kutolewa nje kwa kadi nyekundu daika ya 84.
Katika mchezo huo, kikosi cha Man City
kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Silva, Toure ,
Barry/Dzeko dk90, Nasri/Milner dk54, Aguero na Tevez/Rodwell dk69.
Wigan: Robles, Boyce, Scharner,
Alcaraz, Espinoza, McCarthy, McArthur, Gomez/Watson dk81, McManaman,
Kone na Maloney. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment