WAZIRI MKUU AUDHURIA MISA YA PAMOJA JIJINI ARUSHA YA KUAGA MAREHEMU WALIOFUNIKWA NA VIFUSI
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia
saini kitabu cha maombolezo alipofika mkoani Arusha leo Kuwapa pole
ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu
katika eneo la Moshono Mkoani Arusha. Maporomoko hayo yametokea jana na
kusababisha vifo vya watu13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa
na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru
Waziri
Mkuu akiwa na wabunge wa Arusha na Meya pamoja na mkuu wa mkoa kwenye
msiba huo mzito. Toka Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless
Lema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulongo, Meya wa jiji la Arusha
Mstahiki Gaudence Lyimo, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari
na Mbunge wa kuteuliwa Catherine Magige
Sehemu ya majeneza ya marehemu katika ibada hiyo maalumu leo
Kiongozi wa dini akiombea marehemu waliofariki kwa kuporomokewa na Moramu
Waziri Mkuu akipeana mkono na Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) alipotembelea eneo la tukio.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda alipowasili mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na
jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo
la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha
vifo vya watu 13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine
amelazwa katika Hospitali ya Maunti meru.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akitoka eneo la tukio katika machimbo ya Moramu
katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana
nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili.
Picha zote na Chris Mfinanga
No comments:
Post a Comment