DKT. SHEIN KUTEMBELEA MIKOA YA ZANZIBAR
Makamo Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi Zanzibar Dkt Ali Muhammed Shein amesema kuwa ataendelea
kukiimarisha na kukienzi Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuulinda Muungano
wa Serikali mbili uliopo.
Kauli hiyo ameitoa katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati akizindua ziara yake ya Mikoa mitano ya Zanzibar.
Dkt Shein ambaye pia ni Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema kuwa kuna kila sababu ya
kukiimarisha chama hicho kutokana na umuhimu wake na kwamba Muungano
uliopo wa Serikali mbili ndio njia bora ya kuendeleza mashirikiano ya
kidugu yaliyodumu kwa muda mrefu.
Amesema kuwa lengo kuu la ziara hiyo
ni kupata taarifa za matukio mbali mbali pamoja na changamoto zilizopo
katika mikoa hiyo zinazohusu CCM.
Aidha amewataka viongozi wa CCM kuwa
na mashirikano mazuri katika kukiimarisha Chama na kuhakikisha kwamba
kinapata ushindi katika kila uchaguzi unaokuja.
Dkt. shein amesema kuwa ana imani na
Chama chake kuibuka mshindi katika chaguzi kutokana Chama hicho kuchagua
uongozi makini ambao utahimili vishindo vya uchaguzi ujao.
Katika hatua nyingine Dkt Shein
aliwataka Wananchi kuendelea kujishughulisha na harakati zao za
kujiletea maendeleo na kuepuka kuvunja sheria za nchi.
"Serikali inataka amani na utulivu kwa
Wananchi wake sambamba na kuimarisha maendeleo kama Malengo ya
Mapinduzi yalivyoelekeza na kwa njia hiyo hatuna budi kuyaenzi
Mapinduzi" alieleza Makamo Mwenyekiti wa CCM.
Katika ziara hiyo Makamo Mwenyekiti
amezindua Tawi jipya la CCM la Vikokotoni, Kikwajuni SACCOS BANK pamoja
na kutoa kadi 270 kwa wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment