AWEP TANZANIA YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

African Women Entreprenuership Programme (AWEP) Tanzania Chapter imezinduliwa rasmi jioni hii katika hoteli ya Double Tree,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda ,pamoja na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt

Hii ni Ngao iliyobidhiwa rasmi na Sylvia Banda ambaye ni balozi na mwenyekiti wa AWEP Zambia ,kudhihirisha kuwa AWEP Tanzania imezinduliwa rasmi kwa kuikabidhi kwa Mgeni rasmi wa Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda na Balozi wa Marekani nchini ,Alfonso Lenhardt

Madam Sylvia Banza, Balozi wa AWEP Zambia akiikabidhi ngao hii katika hafla maalum iliyofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree Hotel jijini Dar es salaam leo jioni, Madam Sylvia Banza naye alikabidhiwa ngao hiyo na na Mama Bill Clinton alipoizindua AWEP Zambia mwaka juzi

Balozi wa Marekani nchini Tanzania , Alfonso Lenhardt, ambao ni wafadhili wa AWEP katika mkakati wake wa kuwakwamua wanawake wajasiriamali wa Afrika akizungumza katika hafla hiyo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Ndugu Abdallah Kigoda akiwasili katika hafla ilofanyika jioni hii, na kuhudhuriwa na wanachama kutoka sehemu mbalimbali nchini, ambao baadhi walikuwa katika mafunzo ya kujifunza ujasiriamali ambao unalengo la kuwafanya wawekezaji

![]() |
Mama Lowasa pamoja na Balozi Mwanaidi Maajar walihudhuria uzinduzi huu wa AWEP Tanzania |

Baadhi ya wanachama wa AWEP Tanzania Chapter katika picha ya pamoja na mgeni rasmi sambamba na Balozi wa Marekani Alfonso Renhardt

burudani ilikuwa toka kwa Makumbusho Traditional Dancers
No comments:
Post a Comment