TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, April 11, 2013

JESHI LA POLISI LAKAMATA MTANDAO WA UHARIFU NCHINI

Mahmoud Ahmad Arusha

Jeshi la polisi mkoani hapa limefanikiwa kuuvunja mpango wauhalifu uliokuwa umeandaliwa na mtandao wa uhalifu wa mikoa ya Dar es salaam na Arusha wakishirikiana na walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Victoria Support Service katika lindo mmoja la ulinzi la kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Ibrahimu Kilongo alisema mnamo tarehe 5-3-2013 walipata taarifa kuwa kuna mpango wa kula njama na kuiba kwenye lindo mmoja la kampuni hiyo ya ulinzi kiasi kikubwa cha fedha ndipo walianza kufuatilia na kubaini njama hizo.
Kilongo alisema kuwa walifanikiwa kuzima jaribio hilo na kuwakamata watuhumiwa kadha kutoka kwenye mtandao huo wa uhalifu wanaofanya kwenye mikoa ya Dar es salaam na Arusha na walikiri kutaka kuiba wakishirikiana na walinzi wa kampuni hiyo kwenye lindo mojawapo la kampuni hiyo.
Akiwataja watuhumiwa wa mtandao huo kaimu kamanda kuwa ni Hamad Hassan46 mkazi wa Sanawari,Makanga Ichami 49 mkazi wa Mwanama,Isack Luhanga40 mkazi wa Ngulelo,Johnson Benjamin35 mkazi wa Moshono,na Samwel Daniel28 mkazi wa Daraja mbili huku wakiwataja wenzao wa kutoka Dar es salaam.
Kilongo alisema kuwa huko Usa river kwenye kizuizi cha polisi walifanikiwa kuikamata gari Toyota Carina rangi nyeupe lenye no. za usajili T 734 BSR iliyobeba watuhumiwa kutoka Dar na kuwataja kuwa ni Oscar Mziray47,Samwel Mabiba41,Joseph Zozi22,Ibrahim Kingu49 na Raphael Wiliam28 wote wakazi wa jijini Dar es salaam.
Watuhumia hao pia walikamatwa na mitungi mine ya Gas,Mkasi mmoja mkubwa wa kukatia vitu vizito mitambo miwili ya kuvunjia , pipe moja ya kuunga kwenye mtungi wa Gasi,mabegi manne na mfuko mmoja wa sulphate iliyokuwa itumike kubebea mitungi ya gasi na katika mahojiano walikiri kuja Arusha kufanya uhalifu huo.
Kilongo alisema upelelezi wa tukio hilo bado uanaendelea na kuwa mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika watawafikishi mahakamani kwenda kujibu tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment