TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, April 23, 2013

UPELELEZI KESI YA LWAKATARE UMEKAMILIKA
1 73ee8
Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Issaya Mulungu, amesema upelelezi kuhusu tuhuma za vitendo vya ugaidi zinazomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatale na
mwenzake Joseph Ludovick umekamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mulungu alisema kwa sasa jalada linaandaliwa kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi.
Lwakatare na mwenzake, Ludovick, wanakabiliwa na kesi ya ugaidi, katika Mahakama ya Kisutu. Watu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kufanya mipango ya kumteka na kutaka kumdhuru kwa sumu, Dennis Msacky.
Kuhusu kesi ya kumwagiwa tindikali Kada wa CCM, Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Igunga Septemba 2011, alisema tayari watuhumiwa wawili wamekwishafikishwa mahakamani.
Mulungu alisema kuhusu kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Absalom Kibanda, tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka na matukio mengine yaliyotokea Zanzibar, upelelezi bado unaendelea na kwamba upo katika hatua mbalimbali. Aliwataka watu kuwa na subira:CHANZO MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment