MENGI AVIONYA VYOMBO VYA HABARI
MWENYEKITI wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi, amecharuka na kuvionya vyombo vya habarikuacha kutumika kujenga ajenda zinazohatarisha usalama wa raia na kubomoa amani iliyopo.
Pia amevitaka vyombo hivyo kuacha
kutumiwa na wanasiasa mithili ya kondomu na kugeuka kuwa kioo cha
wakubwa na wenye fedha badala ya kuwa kioo cha jamii.
Dk. Mengi alitoa
onyo hilo jijini Dar es Salaam jana, wakati akifunga mdahalo uliohusu
umuhimu wa waandishi wa habari kushiriki kulinda ya amani
nchini.
Alisema vyombo vya habari, vinatakiwa kujichunguza kabla ya
kuandika na kukuza mambo yanayohatarisha usalama wa nchi.
"Nchi yetu
imejaliwa kuwa rasilimali nyingi sana, lakini amani
inapotoweka ina hatarisha usalama wa
kila mwananchi, hakuna atakayepona, jambo la msingi tuache kulalamika
tuchukue hatua.
"Tunapozungumza chanzo cha uvunjifu wa amani kwa mfano
suala la vurugu za kidini kuhusu kugombania kuchinja, ni suala ambalo
tunaweza kukuta lililetwa na mtu ambaye hata hayupo nchini, hapa
tunahitaji kufanya uchunguzi wa suala hili tusipende kushupalia vitu
ambavyo tunaona kabisa vinaweza kubomoa amani iliyopo.
"Hivi sasa
vyombo vya habari, vimeanza kumeguka na kutumiwa na wakubwa na wenye
nazo, hii ni hali ya hatari sana kwa nchi yetu, kwa sababu badala ya
kuandika habari za wanyonge sasa zimebakia kuwandikwa habari za wakubwa
pekee.
"Tunapaswa kuwa wazalendo... tukumbuke kuwa hawa watu wanalenga
kuwatumia wandishi wa habari kama vile kondom, akishakutumia basi
anakutupa," alisema.
Soma zaidi http://mtanzania.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=6713
No comments:
Post a Comment