WATAALAM WA KILIMO NCHINI WAONGEZEKA WAFIKIA 7,974
Na: Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma
Wataalam
wa ugani wameongezeka kutoka 3,379 waliokuwepo mwaka 2007 hadi kufikia
7,974 mwezi Juni jana(2012) baada ya Serikali kuajiri wahitimu kutoka
vyuo mbalimbali nchini. Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Adam Kigoma Malima wakati akijibu
swali Mhe. Mch. Dk. Getrude Rwakatare (Viti Maalum kupitia Chama cha
Mapinduzi).mAmesema kuwa mwaka 2007 Serikali ilifanya tathmini ya
upatikanaji wa huduma za ugani nchini na kubaini kwamba mojawapo ya
vikwazo vikubwa vya upatikanaji wa huduma za ugani kwa ufanisi nchini ni
upungufu mkubwa wa wataalam.
Malima
ameongeza kuwa matokeo ya tathmini hiyo yalionyesha kuwa kulikuwepo na
wataalam 3,379 nchini ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wataalam
15,082.
Amesema
katika kukabiliana na changamoto hiyo , Serikali ilianza kutekeleza
Mpango wa kuimarisha huduma za Ugani nchini ambapo kuanzia mwaka 2007
Serikali imevifufua vyuo 13 vya kilimo nchini (MATIs) vilivyo chini ya
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.
“Ukarabati
mkubwa wa vyuo vitatu MATI Ukiriguru, Maruku na Naliendele-Mtwara na
ukarabati mdogo kwa baadhi ya vyuo kumi vingine umefanyika”. Mhe. Malima
alisema.
Aidha,
Mhe. Malima amesema kuwa vyuo viwili vya mashirika yasiyo ya kiserikali
vilishirikishwa katika kutoa mafunzo yaliyolenga kuongeza idadi ya
wataalam wa Ugani na vyuo hivo kwa sasa vina uwezo wa kudahili wanafunzi
3,500 kwa wakati mmoja ikilinganishwa na uwezo wa kudahili wanafunzi
600 uliokuwepo kabla ya mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment