FA UINGEREZA YAMFUNGULIA MASHTAKA SUAREZ
Suarez akimng'ata Ivanovic uwanjani:
Chama cha
soka nchini Uingereza, FA kimenuia kumpa adhabu kali mshambuliaji wa
Liverpool Luis Suarez kwa kitendo chake cha kumng'ata beki wa Chelsea
Branislav Ivanovic katika mchezo wa jumapili baina ya Liverpool na
Chelsea,mchezo uliomalizika kwa sare ya 2-2.
FA imesema mwamuzi wa mchezo huo
hakukiona kitendo hicho uwanjani lakini marejeo ya picha za mchezo huo
zilionyesha Suarez alimng'ata Ivanovic,kitendo ambacho kinachukuliwa
kama vurugu mchezoni na adhabu yake ni kufungiwa mechi tatu lakini
adhabu hiyo haitoshi kwa tukio alilolifanya Suarez.
Suarez amepewa muda wa mpaka saa 12
jioni jumanne ya April 23, awe amekubali au kukataa kosa hilo kabla ya
tume ya kudhibiti maadili haijakutana hapo siku ya jumatano kutoa hukumu
stahili kwa kosa hilo.
Mwenyewe Suarez aliisha kiri kufanya
kosa hilo na kumuomba Ivanovic msamaha kwa njia ya simu na kuwaomba
mashabiki wa soka wamsamehe kwa kosa hilo.
Klabu yake ya Liverpool imempa adhabu ya kumpiga faini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay.
Mwaka 2010, Suarez wakati akiichezea
Ajax ya Uholanzi alimng'ata begani kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal
na kufungiwa mechi saba na chama cha soka nchini Uholanzi kwa kosa
hilo.
Itakumbukwa Suarez tayari
amekwishawahi kufungiwa kutocheza mechi nane za mashindano nchini
Uingereza na faini ya paundi elfu 40 kwa kosa la kumtolea lugha ya
kibaguzi beki wa Manchester United Patrice Evra mwaka 2011
:CHANZO BBC
:CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment