MAMLAKA YA MAWASILIANO NA MAKAMPUNI YA SIMU WATOA TAMKO
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof JOHN NKOMA mapema leo asubuhi akitoa tamko juu ya usajili wa namba za simu za mkononi.
Mkurugenzi wa Vodacom RENE MEZA akisisitiza umuhumu wa kusajili namba za simu za mkononi.
Mkurugenzi wa Airtel SUNIL CALASO akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya tamko la usajili wa namba za simu za mkononi.
Mkurugenzi wa Zantel PRATAP GHOSE akizungumzia juu ya tamko la pamoja kuhusu usajili wa simu za mkononi.
Mapema leo asubuhi mkurugenzi wa
mamlaka ya mawasiliano nchini ametoa tamko la pamoja lililo azimiwa kwa
kushirikiana na makampuni ya simu kwamba watumiaji wote wa simu za
mkononi ambao hawaja sajili namba zao wafanye hivyo mara moja,kwani
utaratibu unao fuata hivi sasa ni kufunga namba zote ambazo hazija
sajiliwa,
Akifafanua zaidi amesema kwamba ni
kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyo sajiliwa na adhabu yake ni
faini ya shilingi laki tano au kifungo cha miezi mitatu jela.
Mwisho amewataka wananchi kuhakiki
usajili wao kwa kupiga namba nyota 106 alama ya reli kutoka katika simu
zao za mkononi kwa mtandao wowote.
mtumiaji utapata ujumbe wa taarifa zako za usajili,na kama taarifa si sahihi tafadhali wasiliana na kampuni husuka haraka sana.
No comments:
Post a Comment