USD 117 M ZIMETENGWA KWA AJILI YA BAJETI YA JUMUIYA YA AFIRKA MASHARIKI
Mahmoud Ahmad Arusha
Jumla ya
kiasi cha dola za marekani million 177,238,966 zimetengwa kwenye bajeti
ya jumuiya ya Afrika ya mashariki kwa mwaka wa fedha 2013-14 na
kuidhinishwa na baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo kwenye kikao chao cha
26 dharura kilichoisha leo(jana) jijini hapa. Mbali ya bajeti hiyo;
mkutano
huo ulioanza mnamo tarehe 22-23 kwa ngazi ya wataalamu na kufuatiwa na
mkutano wa makatibu wakuu wa nchi wanachama na kupokea hatua
zilizofikiwa katika majadiliano ya itifaki ya umoja wa fedha wa jumuiya
ya Afrika ya mashariki ambao unatarajiwa kutiwa saini na wakuu wa
jumuiya hiyo katika mkutano wao wa 15 mwezi wa november mwaka huu.
Aidha
mkutano huo utajadili pia pendekezo la kuongeza wigo wa mamlaka ya
mahakama ya Afrika ya mashariki kwa kupitia mapendekezo yaliojadiliwa
kwenye vikao vya wataalamu na makatibu wakuu wa jumuiya hiyo.
Katika
hatua nyingine mkutano huu wa dharura wa 26 wa jumuiya ya Afrika ya
mashariki ambao unaisha leo na kuwakutanisha wataalamu na makatibu wakuu
kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrka ya mashariki umejadili mambo
matatu makuu yatakayopelekwa kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa jumuiya
hiyo kwa ajili ya kutia saini.
Kwa
upande mwingine mkutano huu umejadili pia hatua iliyofikiwa katika
uandaaji wa itfaki ya hadhi na kinga kwa watumishi wa jumuiya na taasisi
zake zote.
No comments:
Post a Comment