MIKUTANO YA BENKI YA DUNIA IFM WASHINGTON DC
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu akitoa maelekezo kwa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe. Gavana alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha.
Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya (kushoto) akitoa ufafanuzi katika kikao cha pamoja cha wajumbe kutoka Tanzania kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC.
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi Susan Mkapa pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya wa Wizara ya Fedha wakisikiliza kwa makini katika kikao hicho pembeni ni Mchumi mwandamizi wa Wizara ya Fedha Bw. Patric Pima.
Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Msaidizi wa Gavana Bw. Msafiri Nampesya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman Saleh wakisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na IMF Bw. Paul Mwafongo.
Wajumbe wakisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na Gavana wa Benki Kuu hayumo pichani, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dr. Joseph Masawe, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango.
No comments:
Post a Comment