VURUGU ZAZUKA CHUONI ARUSHA BAADA YA MWANAFUNZI KUCHOMWA KISU NA KUFARIKI
*CAUTION/ILANI: Taarifa hii ni ya
awali kutoka kwa watu mbalimbali. Unafahamishwa tu kuwa na ufahamu wa
kinachoendelea. Taarifa kamili na iliyo rasmi itatolewa na vyombo
husika.
---
---
Taarifa katika mitandao jamii
zinaeleza kwamba usiku wa kuamkia leo, kijana mmoja wa kiume ambaye ni
mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (Arusha Institute of Accountancy)
aliyekuwa anasomea shahada ya kwanza Uchumi na Fedha (Bachelors Degree
in Economic and Finance) mwaka wa pili (BEF2), amefariki dunia baada ya
kuchomwa kisu.
Taarifa za awali kutoka chuoni hapo ambazo bado hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi zinaeleza kwamba kijana huyo anahisiwa kuchomwa kisu na vibaka wakati akirejea kwenye maeneo yao ya malazi (hosteli) eneo la ESAMI.
Inaelezwa kuwa, kabla ya kufika hostel, alipigiwa simu na mwenziye kuwa amsubiri ili waongozane pamoja kuelekea hostel. Wakati akisubiri rafiki yake amfikie, ndipo watu wasiofahamika waliokuwa wanadai wapatiwe fedha, walimvamia na kumchoma kisu tumboni na shingoni.
Rafiki wa marehemu naye pia alichomwa kisu tumboni.
Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Godbless Lema alifika chuoni hapo na kuzungumza na wanafunzi hao ili kuwatuliza baada ya kutaarifiwa kuwa kuna vurugu zilizotokana na hasira ya Wanachuo kumshutumu Mkuu wa Chuo kutokuwapa msaada wa haraka hasa baada ya wao kulalamika kwa muda mrefu sasa kuhusu hali duni ya usalama katika chuo hicho. Mwaka jana mwanafunzi mmoja aliuawa na katika nyakati tofauti, wanafunzi wamekuwa wakivamiwa na kuibiwa vifaa vyao.
Taarifa pia zilimfikia Mkuu wa Mkoa, Magessa Mulongo ambaye aliwasili chuoni hapo na kuzungumza na wanachuo lakini ilizuka tafrani ndipo Wanachuo walianza kurusha mawe.
Kikosi maalumu cha Askari Polisi wa kutuliza ghasia, FFU, kipo katika eneo hilo kwa ajili ya kufanya kazi yake.
CHANZO:WAVUTI
No comments:
Post a Comment