"HATUOGOPI VITISHO VYA WAASI WA M23....NI LAZIMA TUPELEKE JESHI DRC"....WAZIRI MEMBE
Dar
es Salaam haitarudi nyuma katika kupeleka majeshi huko Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kama sehemu ya kikosi cha kuingilia kati cha
Umoja wa Mataifa, licha ya maonyo mawili ya maandishi kutoka kikundi
cha waasi cha March 23rd Movement (M23), maafisa wa Tanzania wasema.
Waasi
wa M23 wakiondoka toka milimani tarehe 30 Novemba, 2012, baada ya
kuondoka kijiji cha Karuba cha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo. [Na Phil Moore/AFP]
Salva
Rweyemamu, mkurugenzi wa mawasiliano wa raisi wa Tanzania, aliiambia
Sabahi kuwa serikali ilipokea barua mbili kutoka kikundi cha M23,
ambacho kinapigana ili kuiangusha serikali ya Kongo.
Barua
ya kwanza ilielekezwa kwa Mwenyekiti Mkutano wa Kimataifa wa Maziwa
Makuu, Raisi wa Uganda Yoweri Museveni, na nyakala kupelekwa kwa wakuu
wote wa serikali wa kanda hiyo, akiwemo Raisi wa Tanzania Jakaya
Kikwete.
Barua
ya pili ilitumwa kwa spika wa Bunge la Taifa Anne Makinda na kutiwa
saini na Bertrand Bisimwa, mkuu mpya wa tawi la kisiasa la M23,
iliyofika bunge la Tanzania siku ya Jumamosi (tarehe 20 Aprili), vyanzo
viliiambia Sabahi.
Mkuu
wa kijeshi wa M23 Jenerali Sultani Makenga (katikati) akiwaashiria
baadhi ya maafisa wake karibu na mji wa Sake, mashariki ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 30 Novemba, 2012. [Na Phil Moore/AFP]
Katika
barua hiyo, M23 iliwataka wabunge wa Dar es Salaam kuishauri serikali
dhidi ya kupeleka majeshi huko DRC, na hata kutishia "mauaji" ya majeshi
ya Tanzania na wapiganaji wa M23 ikiwa Tanzania itaendelea mbele na
upelekaji wa majeshi yake huko.
Kurejesha amani
"Lengo
la majeshi ya Tanzania sio kuwaua Wakongo bali kurejesha amani," naibu
Spika wa Bunge la Taifa la Tanzania Job Ndugai aliiambia Sabahi. "M23
wataona hili kuwa ni tatizo ikiwa hawataki amani. Hatupeleki askari wetu
kwenda kuua au kuuliwa na M23."
Hapo
tarehe 28 Machi, Baraza la Usalama la UN kwa kauli moja lilipitisha
Azimio 2098, ambalo lilisafisha njia kwa chombo cha kwanza cha kimataifa
cha kikosi cha "mashambulizi". Mamlaka ya kikosi hicho cha kuingilia
kati, itakayoundwa na vikosi vya askari wa miguu kutoka Tanzania, Afrika
Kusini, Msumbiji na Malawi, ni "kuwamalizia nguvu na kuwanyang'anya
silaha" wa M23, waasi wa Kongo na vikundi vyenye silaha vya kigeni huko
mashariki ya DRC, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Umoja wa
Mataifa.
Katika barua ya tarehe 11 Aprili, Bisimwa alionya kwamba M23 itaishinda kikundi cha UN itakachoongozwa na jenerali wa Tanzania.
Mnamo
tarehe 7 Aprili, Bisimwa alitoa vikosi kama hivyo kwa majeshi ya Afrika
Kusini katika akaunti yake ya Twitter, lakini Afrika Kusini ilisema
kuwa itaendelea na mipango yake ya kujiunga na kikosi cha uingiliaji
kati cha UN huko DRC.
Kwa
majibu ya barua ya Bisimwa kwa Spika Makinda, Azimio 2098
"linabadilisha Misheni ya UN ya Kulinda Amani huko DRC na kuifanya kuwa
kikosi cha vita chenye amri ya kufanya operesheni za mashambulizi dhidi
ya wananchi wa Kongo".
Bisimwa,
ambaye anaushutumu Umoja wa Mataifa kwa kuingilia kati DRC kwa ajili ya
kuiokoa serikali ilioko madarakani, kiliapa kuwa vikosi vya M23
vitaishinda kikosi cha uingiliaji kati.
Alisema
kuwa anamheshimu sana raisi wa kwanza wa Tanzania, marehemu Mwalimu
Julius Nyerere, lakini bado M23 itakuwa haina chaguo jengine bali
"kuyaua majeshi ya ndugu zao kutoka Tanzania".
Kanali
Kapambala Mgawe, msemaji mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi la
Tanzania, alirudia kusema kuwa vikosi vya Tanzania vinakwenda Mashariki
mwa DRC kuleta amani katika eneo hilo.
"Ambapo
maisha ya wananchi wa DRC au walinda amani itakuwa katika hali ya
hatari, vikosi vyetu vitaokoa maisha na kuwanyang'anya silaha wale
wanaosababisha hatari hiyo," aliiambia Sabahi. "Huu ni msimamo na
maelekezo kutoka UN."
Vitisho huko nyuma
Waziri
wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Bernard Membe aliiambia Sabahi
kuwa Tanzania imezowea kupokea vitisho kama hivyo visivyo na msingi
kutoka vikundi vya waasi kila mara majeshi yake yanapoingilia kati
kuwaokoa watu wasio na hatia.
Kama
mfano, alitaja uingiliaji kati kijeshi wa Umoja wa Afrika huko Anjuan,
katika visiwa vya Komoro, ambao ulimuondoa madarakani raisi wa zamani
Kanali Mohamed Bacar. Licha ya vitisho kama hivyo dhidi ya mchango wa
majeshi kutoka Dar es Salaam, vikosi vya Tanzania havikurudi nyuma,
Membe alisema.
"Nadhani
wao [M23] wangemuenzi Mwalimu Nyerere kwa kumaliza vita vya wenyewe kwa
wenyewe ambavyo vinasababisha ubakaji uliotapakaa, vifo vya watoto na
wanawake, na watu wanaokimbia makazi yao," alisema.
Membe
alisema M23 kinapaswa kumaliza uasi wake na kuacha kuua watu wasio na
hatia, kwa hivyo kutoipa Tanzania sababu yoyote ya kupeleka kikosi chake
DRC.
No comments:
Post a Comment