BALOZI SEIF NA WIKI YA USALAMA BARABARANI ZANZIBAR
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar
Imeelezwa
kuwa ikiwa kutakuwa na ushirikiano na uadilifu baina ya watoaji
leseni za Udereva na Jeshi la Polisi nchini itapelekea kupunguza ajali
za Baraabarani zisizokuwa za lazima.
- yameelezwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi, Wanafunzi pamoja na Madereva wa vyombo vya moto kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabani katika ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar .
- Seif amesisitiza Umakini katika utoaji wa leseni na kuwataka Madereva kufuata Sheria wakati wanapoendesha vyombo ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika kwa wananchi wanaotembea kwa miguu na wale wanaoendesha vyombo vidogo vidogo.
“Katika
kuyafikia malengo ya mpango wa miaka kumi ya usalama barabarani natoa
wito kwa madereva kutoendesha mwendo wa kasi wanapokuwa barabarani,
kutii sheria, kuwajali watumiaji wengine wa barabara ikiwa ni pamoja na
waenda kwa miguu, wapanda baskeli na watu wenye mahitaji maalum” Alisema
Makamu wa pili wa Rais.
Ameahidi
kuwa Serikali kwa upande wake itahakikisha kuwa inasimamia kwa
ukamilifu sheria za barabarani na kuwachukulia hatua wale wote wanao
kaidi kufuata sheria hizo.
Ameongeza
kuwa Serikali itahakikisha kuwa barabara zinazojengwa zinakidhi viwango
ikwa ni pamoja na uimara wa barabara zenyewe , upana pamoja na kuwekwa
alama zote muhimu zinazohusu usalama wa barabarani.
Nae
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa amesema ni vyema
kamati ya mawasiliano kulishirikisha Jeshi la Polisi wakati
wanapotoa maamuzi katika masuala ya ujenzi wa barabara ili na wao
waweze kutoa mchango wao kabla ya ujenzi kuanza.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dokta Ahmed Jidawi ameshauri madereva kufanyiwa
uchunguzi wa kiafya kabla ya kupatiwa leseni kama vile kuchunguzwa
akili na hata macho jambo ambalo litapelekea kupata madereva walio
bora .
Mkurugenzi
wa Miundo mbinu na Mawasiliano amekemea tabia mbaya inayofanywa na
baadhi ya watu kuondoa alama za barabarani na kusema kwamba serikali
itawachukulia hatua watakaobainika kufanya vitendo hivyo.
Aidha
amewanasihi madereva kuwa makini na kupunguza matumizi ya simu wakati
wanapoendesha gari kwani ni miongoni mwa vichocheo vya kutokea ajili za
barabarani.
Kauli mbiu ya wiki ya usalama barabarani mwaka huu ni ‘’KUONDOA AJALI ZA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE’’.
No comments:
Post a Comment